AFYA NA KIASI SIKU YA 18
KIZOTA NET EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE*
23/06/2021, SIKU YA 18
AFYA NA KIASI
Na Dkt. DANIEL MTANGO & ELIZABETH
*_SOMO: PUMZIKO_*
Pumziko ni amri ya saba katika amri za afya.
Kupumzika ni kuacha kufanya kazi hasa zile kazo za kawaida.
Sio lazima kulala lakini kumbuka kulala usiku kwani usiku umewekwa kwa ajili ya kupumzika. Unaweza kutembea bustanini n.k.
Kupumzika ni agizo kutoka kwa Mungu
Kutoka 20:8-11
Kutoka 20:8
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Kutoka 20:9
Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
Kutoka 20:10
lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
Kutoka 20:11
Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
Hatua za kulala usingizi mzuri:-
1. Pre sleep (kabla ya kulala andaa mazingira)
2. Mapigo ya moyo yanapungua
3. Misuli inapumzika
4. Macho yanaenda upande na kuzunguka
5. Anaota ndoto nzuri
* Ndoto mbaya ndiyo zinazotokana na kushiba sana.
* Ndoto nzuri/njozi nzuri ndizo zinakuja baada ya kupata usingizi mzuri.
UMUHIMU WA KUPUMZIKA
1. Usipopumzika utaugua
Usichoshe mwili wako, kumbuka Mungu ametoa siku maalum ya kupumzika ambayo ni siku ya saba. Kutoka 20:8-11.
2. Wengi wanachanganyikiwa kutokana na kutopumzika
Tumbo, mapafu, na viungo vingine vinatakiwa kupumzika.
Mapendekezo:
+ Lala mapema kabla ya saa 3 na kuamka mapema. Na lala angalau masaa 8-9. Tumia angalau nusu saa kulala mchana.
+ Watoto wadogo wanatakiwa kulala mchana angalau masaa 2.
+ Hacha kunywa vinywaji vinavyoondoa usingizi na hacha kuangalia michezo na tamthilia usiku.
+ Kula chakula chepesi usiku na kula mapema.
DENI LA USINGIZI
Ukikosa usingizi kwa saa 1 kila siku kwa siku 7 unapoteza saa 7 Sawa na siku moja nzima ya kulala.
* Unapunguza kinga yako ya mwili na kuleta magonjwa
* Ajali nyingi zinatokana na madereva kukosa usingizi.
* Unaongeza kupunguza kumbukumbu nzuri ya akili na kuongeza msongo wa mawazo.
TIBA YA KULETA USINGIZI
1. Usipende kutumia madawa haya hayaleti usingizi mzuri.
2. Jitahidi kulala saa ileile kila siku
3. Fanya mazoezi mepesi
4. Lala kwenye chumba chenye madirisha makubwa na inayoingiza hewa.
Mhubiri 5:12
Usingizi wake kibarua ni mtamu, kwamba amekula kidogo, au kwamba amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi.
5. Oga maji moto, husaidia mishipa kuwa sawa.
6. Epuka kazi ya kuketi sana
7. Lala mapema kila siku.
8. Fanya ibada kabla ya kulala
Mathayo 11:28-29
Mathayo 11:28
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Mathayo 11:29
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
9. Usilale na hatia/wasiwasi.
Waefeso 4:26
Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;
*TUBARIKIWE SOTE, KARIBU TENA KESHO.*
☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆
Post a Comment