MUSEVENI AMTEUA MUHOOZI KAMANDA WA MAJESHI YA ARDHINI

Gumzo mojawapo Nchini Uganda ni uamuzi wa Rais Museveni (76) kumteua Mtoto wake Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba (47) kuwa Kamanda wa majeshi ya ardhini, hii imepigilia msumari headline za Jenerali huyu kuandaliwa kurithi Urais Baba yake atakapostaafu.

Rais Museveni ameitawala Uganda kama Rais tangu mwaka 1986 ambapo licha ya Mtoto wake huyu kuwa kwenye nafasi za juu za ulinzi wa Nchi na Rais, Mke wake Janet Museveni (72) amekua Waziri kwenye Wizara mbalimbali tangu mwaka 2009.

No comments