NENO KUU LEO SIKU YA 16
KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE- SIKU YA 16*
NENO KUU
Pastor. Mark Walwa Malekana
SOMO: SHERIA ILIYOISHIA MSALABANI_*
Mathayo 11:28, 29
Mathayo 11:28
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Mathayo 11:29
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu
Moja ya mijadala ulimwenguni leo ni pamoja na sheria zilizokoma msalabani. Katika Biblia vitabu 5 vya Musa vina sheria 613. Zimegawanyika katika makundi mawili
1. Sheria za Mungu na
2. Sheria za Musa
Sheria za Mungu ni zile Amri kumi (10) yaani sheria za maadili, zingine zote zilizobaki zilikuwa sheria za Musa.
Kwanini tutii Amri za Mungu?
Mafanikio yote ya mwanadamu yamejengwa kwenye kumsikiliza Mungu.
Zaburi 1:1-3
Zaburi 1:1
Heri mtu yule asiyekwenda, Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Zaburi 1:2
Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
Zaburi 1:3
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Zaburi 128:1-6
Zaburi 128:1
Heri kila mtu amchaye BWANA, Aendaye katika njia yake.
Zaburi 128:2
Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.
Zaburi 128:3
Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.
Zaburi 128:4
Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA.
Zaburi 128:5
BWANA akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
Zaburi 128:6
Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.
Sheria zote za Mungu hazikuishia msalabani.
Sifa za sheria za Mungu
Sheria za Mungu zina sifa hizi:-
1. Ilinenwa na Mungu mwenyewe
Kumbukumbu la Torati 4:12
BWANA akasema nanyi kutoka kati ya moto; mkasikia sauti ya maneno, lakini hamkuona umbo lo lote; sauti tu.
2. Iliandikwa na Mungu juu ya mbao za mawe
Kumbukumbu la Torati 10:1
Wakati ule BWANA akaniambia, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, kisha uje kwangu huku mlimani, ukajifanyie na sanduku la mti.
Kumbukumbu la Torati 10:2
Nami nitaandika juu ya hizo mbao maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, ulizozivunja, nawe uzitie ndani ya hilo sanduku.
Kumbukumbu la Torati 10:3
Basi nikafanya sanduku la mti wa mshita, nikachonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, nikakwea mle mlimani, na zile mbao mbili mkononi mwangu.
Kumbukumbu la Torati 10:4
Naye akaandika juu ya mbao mfano wa maandiko ya kwanza, zile amri kumi, alizowaambia BWANA huko mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano; BWANA akanipa.
3. Iliwekwa kwenye sanduku la agano
Kumbukumbu la Torati 10:5
Basi nikageuka nikashuka kutoka mlimani, nikazitia mbao ndani ya sanduku nililofanya; nazo zimo humo kama alivyoniamuru BWANA.
4. Kazi yake ni kuonesha uhusiano wa wanadamu sisi kwa sisi na kati ya mwanadamu na Mungu, ikiwekwa katika Upendo.
Sifa za sheria za Musa
1. Ziliandikwa na Musa mwenyewe
Kumbukumbu la Torati 31:9
Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, wana wa Lawi, waliolichukua sanduku la agano la BWANA, na wazee wote wa Israeli.
2. Iliandikwa kwenye chuo (kitabuni)
Kumbukumbu la Torati 31:24
Basi ikawa hapo Musa alipomaliza kuandika maneno ya torati hii katika chuo, hata yakaisha,
3. Iliwekwa nje( kando ya sanduku la agano)
Kumbukumbu la Torati 31:26
Twaeni chuo hiki cha torati, mkiweke kando ya sanduku la agano la BWANA, Mungu wenu, ili kiwepo kama shahidi juu yako.
4. Ilielekeza ujio wa Yesu
Katika sheria ya Musa kulikuwa na sabato nyingi (sikukuu nyingi) ambazo ndizo ziliisha.
Wakolosai 2:14-17
Wakolosai 2:14
akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
Wakolosai 2:15
akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
Wakolosai 2:16
Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
Wakolosai 2:17
mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
5. Inaitwa sheria ya Musa
Malaki 4:4
Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.
6. Ilidumu mpaka Kristo alipokufa msalabani
Waebrania 9:10,11
Waebrania 9:10
kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.
Waebrania 9:11
Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu,
7. Iliondolewa na msalaba
Waefeso 2:15-17
Waefeso 2:15
Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani.
Waefeso 2:16
Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.
Waefeso 2:17
Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu.
8. Ilikuwa kivuli ya huduma ya Yesu, Waebrania 9:10-12
*SHERIA ZILIZOKOMA MSALABANI NI ZIPI?*
1. Sheria za kafara na ibada hekaluni.
2. Mapumziko ya kitaifa (ambazo zilitajwa kama sabato Wakolosai 2:14-17)
Lakini Sabato ya amri ya nne ipo palepale
Waebrania 4:9
Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.
3. Sheria za uraia (mfano:- ukikosea ilikuwa unapondwa mawe mpaka kufa)
4. Sheria za utakaso (mfano:- wanawake wakiwa katika siku zao walitengwa, wenye ukoma n.k)
5. Tamaduni (mfano:- kutahiriwa na kuvua viatu n.k)
*Mungu anatuita tufanye nini?*
Waebrania 8:1,2
Waebrania 8:1
Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,
Waebrania 8:2
mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.
Tumtazame Mwanakondoo wa Mungu, Yesu Kristo yupo kwa ajili yetu kutusaidia kuishinda dhambi.
*TUBARIKIWE SOTE, KARIBU TENA KESHO*
Post a Comment