• HOME
  • BREAKING NEWS
  • TAMTHILIA
  • MICHEZO
  • MATANGAZO
  • CONTACT US

BINAGO BLOG

  • Home
  • Home / Habari / MWELI AWAONYA MAAFISA ELIMU

    MWELI AWAONYA MAAFISA ELIMU

    Bisaya Raphael June 09, 2021 Habari
    OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imesema haitasita kumchukulia hatua Afisa Elimu wa Wilaya na Mkoa atakayeshindwa kuzitumia fedha za Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) zilizopelekwa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu.

    Aidha, Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wameagizwa kuanza mara moja utekelezaji wa ujenzi wa madarasa kwenye maeneo yao yanayojengwa kupitia EP4R.

    Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli ametoa agizo hilo katika hafla ya ufungaji mafunzo ya Uthibiti Ubora wa Shule wa Ndani kwa Maafisa elimu wa Mikoa, Wilaya na Maafisa Elimu taaluma wa Mikoa yote nchini.

    Mweli amesema fedha hizo tayari zimeshapelekwa kwenye Halmashauri hizo mwishoni mwa mwezi Aprili, mwaka huu na kuataka ujenzi ukamilike kwa wakati.

    “Kuna Halmashauri zaidi ya 60 hadi sasa hazijaanza ujenzi wa madarasa kupitia fedha za EP4R zilizoletwa na Serikali katika maeneo yenu, nawaagiza kwenda kutekeleza na kusimamia ujenzi huu wa madarasa na baada ya wiki mbili tutafanza ziara za kukagua ili kuona ujenzi huu unavyoendelea, kila Halmashauri iwe imeanza ujenzi huu wa madarasa na mhakikishe inakamilika kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa na ni lazima ikamilike ndani ya miezi mitatu, baada ya muda huo, kila Afisa Elimu Mkoa alete taarifa ya namna miradi hii ilivyotekelezwa hadi kukamilika katika Mkoa wake” amesema Mweli

    Aidha, Naibu Katibu Mkuu Mweli amewataka Maafisa Elimu hao kuhakikisha wanakwenda kuyatumia vizuri mafunzo hayo waliyopatiwa ili kuboresha eneo la Uthibiti Ubora Shule wa Ndani utakaowezesha kuinua na kuimarisha ubora wa elimu ya Msingi Nchini.

    Mafunzo hayo kwa kundi la Walimu Wakuu wa Shule za Msingi 8,799 kwa ufadhili wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia mradi wa GPE – LANES II.

    Related Posts

    Habari

    Post a Comment

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    KWA SHEREHE NA SEMINA KARIBU UKUMBI WA LAKE TANGANYIKA, NZEGA-TABORA

    FOOTBALL STORIES

    Follow us

    • Like on Facebook
    • Follow on Twitter
    • Follow on Instagram
    • Subscribe on Youtube

    Popular Posts

    • kusuka na unyoaji katika Biblia
      kusuka na unyoaji katika Biblia
       KAMA MUNGU ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAWAKE ! NDIVYO ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAUME PIA. BWANA YESU asifiwe!😅 Maranatha!😅🙏🏻 N...
    • Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      *https://youtu.be/-P4s8sVq31o* 🤔🤔🤔🤔🤔 *JE NI HALALI KWA MKRISTO KULIPA MAHARI ILI AOE?????* 🤔🤔🤔🤔🤔 . . . Hebu tutazame k...
    • HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      KANISA LA #SDA LINA MISINGI 28 AMBAYO NI 1.Neno la Mungu 2.Utatu mtakatifu 3.Mungu baba 4.Mungu mwana 5.Roho mtakatifu 6.Uumbaji...

    Labels

    Habari MICHEZO Live injili Tamthilia Kesha la Asubuhi BREAKING NEWS magazeti Matangazo Covid19 Mastaa Viongozi today's quote Lesoni leo Wimbo wa Leo barikiwa Je Wajua? KULFI Bongo Movies Stories TETESI ZA USAJILI

    Facebook

    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates