MCHOPANGA AMSHUKURU RAIS SAMIA
Pili kipekee nimshukuru Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. @samia_suluhu_hassan kwa Kuniamini na Kuniteua kumwakilisha kushirikiana na wenzangu kutatua Changamoto za Wilaya ya Rorya.
Ninatambua jamii ina ya watu wa Rorya Ina mila, desturi na Tamaduni zake.
Lakini huwezi kuwa kiongozi bila kuwepo unaowaongoza, hivyo kuwasikiliza, kuwaelimisha na kujenga muafaka wa pamoja itakuwa ndio dira yangu kubwa.
Kwangu uongozi ni utumishi, nitawatumikia wananchi wote kwa haki, usawa na maridhiano nikitambua bila wao siwezi kuitwa kiongozi.
MUNGU Ibariki Afrika, MUNGU Ibariki Tanzania, MUNGU mbariki Rais wetu Mh Samiha Suluhu Hassan. MUNGU Ibariki Mara, MUNGU Ibariki Rorya.
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano.
-----> Mkuu wa Wilaya wa Rorya, Juma Chikoka Maarufu Chopa Mchopanga.
Post a Comment