PUNGUZO LA BEI FURSA KWA WANANCHI KUUGANISHA UMEME
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na Wananchi Mkoani Lindi Jana Juni 20, 2021 amesema kuwa, punguzo kubwa la bei ya kuunganisha umeme mpaka kufikia Shilingi 27,000, imekuwa njia nzuri na fursa kwa Watanzania wote kuunganisha Umeme.
“Punguzo hili la bei litawezesha Watanzania kuendana na lengo la Serikali la kuwezesha Watanzania wote kufikiwa na kuunganisha huduma ya Umeme kwa maeneo yote ya Mijini na Vijijini” alisema Dkt. Kalemani
Dkt. Kalemani ameeleza kuwa, punguzo hilo kubwa la gharama za kuunganisha umeme pia litawezesha Watanzania wa vipato vyote kumudu gharama za kuunganisha umeme na kuutumia kwa ajili ya kujikwamua kimaendeleo ikiwemo maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa maeneo yote ya Mijini na Vijijini.
Aidha, Dkt. Kalemani akizungumza na Wananchi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara katika mikutano miwili tofauti iliyofanyika mikoani humo mwishoni mwa wiki, ameelezea mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uboreshaji wa huduma za Umeme katika mikoa hiyo ya kusini mwa Tanzania, kutokana na Miradi mikubwa ya uboreshaji wa Miundombinu ya kusambaza na kusafirisha umeme katika mikoa hiyo.

Post a Comment