MTOTO MDOGO ANYONGWA NA MFANYAKAZI WA NDANI

ACPJustin Masejo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, amewafahamisha wanahabari kuwa mnamo tarehe 19/6/2021 majira ya saa 12:00 jioni huko maeneo ya olasiti katika jiji la Arusha, mtoto mdogo aliyefahamika kwa jina la TIFAN S/O OSWARD mwenye mwaka mmoja na nusu
aliuawa kwa kunyongwa shingo na msaidizi wa kazi za ndani jina limehifadhiwa ambaye aliachwa nyumbani na mtoto huyo.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa binti huyo aliajiriwa miezi miwili iliyopita akitokea Mkoa wa Mara. 

Jeshi la Polisi linaendelea kufanya Upelelezi ili kubaini chanzo cha tukio hilo, Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi kufahamu chanzo cha maamuzi hayo na pindi Upelelezi utakapo kamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa uamuzi wa kisheria.

Aidha ACP Justin Masejo ameomba atoe wito kwa wazazi na walezi kufuatilia mienendo ya wasaidizi wao wa kazi za ndani kabla na baada ya kuwachukua ili iwasaidie kufahamu tabia zao kwa kina na pindi wanapowachukua wasaidizi hao yasitokee madhara yeyote kwa watoto na familia zao pindi wanapowaachwa majumbani.

No comments