• HOME
  • BREAKING NEWS
  • TAMTHILIA
  • MICHEZO
  • MATANGAZO
  • CONTACT US

BINAGO BLOG

  • Home
  • Home / MICHEZO / ALI KAMWE; YANGA WAKIBADILIKA KUNA FUTURE MBELENI

    ALI KAMWE; YANGA WAKIBADILIKA KUNA FUTURE MBELENI

    Bisaya Raphael June 21, 2021 MICHEZO
    Ndani ya siku 3, Yanga wamecheza mechi 2. Dhidi ya Ruvu Shootings na Mwadui FC

    Mwadui tayari wameshuka daraja. Ruvu ana pointi 37. Tofauti ya pointi 2 na timu inayoshika nafasi ya kuteremka daraja moja kwa moja msimu huu

    Kwenye hizo dakika 180, Yanga wamepata pointi 6, wakifunga Mabao 6 na kufungwa mabao 4

    It's true, wamepeta pointi 6 lakini wengi walitarajia Yanga wapate ushindi wakiwa 'comfotabo', na hii ni kutokana na aina wapinzani aliokutana nao

    Lakini tusisahau, na sio kwa Tanzania tu, katika dunia ya Football, nyakati kama hizi timu zilizokuwa kwenye hatari ya kushuka daraja huwa hatari sana. 

    Kwanini? Ziko sababu mbili

    1: Kwa 'Underdogs', It's Do or Die kwao hivyo tegemea kuona Intensity ya mechi ikipanda. Tegemea kuona wakikimbia kilomita nyingi huku morali ikiwa juu.

    2: Kwa Top Clubs, wachezaji huathirika kwa kiasi fulani kisaikolojia. Mara nyingi huanza mechi kwa kasi ndogo bila Tahadhari . Hii ni kwa sababu ya kuamini wanacheza na mpinzani dhaifu, hivyo bao litakuja tu. 

    Kwa lugha rahisi, mashabiki husema 'Walidharau mechi'. Ni mtego huu wa Kisaiokolojia ambao hunasa Top Clubs nyingi duniani katika mazingira ya mwisho wa msimu.

    Hivyo, kama kuna mahala ambapo unaweza kuwalaumu Yanga ni kitendo chao cha kuwa re active na sio pro active.

    Mbali na hapo, Kuna 'positivity' nyingi sana za kutazama kwenye kikosi cha Yanga. 

    Tactically, timu imebadilika. System iko better na style of play ni Fantastic sana. Makosa mengi yaliobaki ni ya wachezaji binafsi.

    Na hapa ndipo unapoona viongozi wakipambana kwenye dirisha la usajili kuboresha ubora katika baadhi ya maeneo

    Kuna kitu mwalimu Nabi ameanza kukipanda kwenye kikosi. Timu inatengeneza nafasi nyingi, zinazojirudia katika style moja. 

    Dhidi ya Mwadui, Yanga wametengeneza nafasi 10+. Dhidi ya Ruvu ni 8+. Kwenye wastani wa nafasi 18 kwa mechi 2 na kufunga mabao 6, hapa unaamini kama Yanga wangekuwa na mastraika wakatili, hizi mechi zingeisha kwa ushindi mnono.

    Kama wataendelea kushinda, kujiamini kukarudi kwa baadhi ya wachezaji, Uongozi ukaboresha ubora baadhi ya maeneo, kuna Future nzuri.

    Related Posts

    MICHEZO

    Post a Comment

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    KWA SHEREHE NA SEMINA KARIBU UKUMBI WA LAKE TANGANYIKA, NZEGA-TABORA

    FOOTBALL STORIES

    Follow us

    • Like on Facebook
    • Follow on Twitter
    • Follow on Instagram
    • Subscribe on Youtube

    Popular Posts

    • kusuka na unyoaji katika Biblia
      kusuka na unyoaji katika Biblia
       KAMA MUNGU ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAWAKE ! NDIVYO ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAUME PIA. BWANA YESU asifiwe!😅 Maranatha!😅🙏🏻 N...
    • Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      *https://youtu.be/-P4s8sVq31o* 🤔🤔🤔🤔🤔 *JE NI HALALI KWA MKRISTO KULIPA MAHARI ILI AOE?????* 🤔🤔🤔🤔🤔 . . . Hebu tutazame k...
    • HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      KANISA LA #SDA LINA MISINGI 28 AMBAYO NI 1.Neno la Mungu 2.Utatu mtakatifu 3.Mungu baba 4.Mungu mwana 5.Roho mtakatifu 6.Uumbaji...

    Labels

    Habari MICHEZO Live injili Tamthilia Kesha la Asubuhi BREAKING NEWS magazeti Matangazo Covid19 Mastaa Viongozi today's quote Lesoni leo Wimbo wa Leo barikiwa Je Wajua? KULFI Bongo Movies Stories TETESI ZA USAJILI

    Facebook

    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates