MBWA ANAESAIDIA WAATHIRIWA WA UHALIFU MAHAKAMANI
Mahakama moja nchini Ufaransa ina Mbwa anayekuwa mahakamani kwa ajili ya kusaidia waathiriwa wa uhalifu kuondoa wasiwasi.
Mbwa huyu kwa jina Lol mwenye umri wa miaka mitano, amekuwa mahakamani kwa muda wa miaka miwili sasa akifanya kazi hiyo.
Mbwa huyu mweusi hutembea na waendesha mashitaka, huku akitoa usaidizi wa kisheriakwa waathiriwa wa uhalifu, hususan wale ambao waliathiriwa na unayanyasaji wa kingono na unyanyasaji mwingine.
"Baada ya kumhoji muathiriwa huwa ninamuita mbwa kusaidia kama ninaaminiuwepo wake utasaidia kumliwazaili aweze kufunguka na kusema kilichotokea, au hata wanapolazimika kutoa ushahidi wakati mahakamani ," anasema Mwendesha mashitaka Frédéric Almendros. "Mbwa huketi kando ya waathiriwa mahakamani na mara nyingi huwasaidia kuhimili wasi wasi mahakamani."
Lol anadhaniwa kuwa ndiye mbwa wa kwanza baraniUlaya kutoa usaidizi wa aina hii mahakamani na anaamimiwa kuifahamu mahakama kuliko mhalifu yeyote sugu.
Amefundishwa kuwa mtulivu
Mbwa huyu aina yaLabrador amefundishwa kuwa mtulivu anapowaona watu asio wafahamu, wakiwemo watoto. Anaweza kutulia hata wakati wa wasiwasi ,hali zinazowafanya watu mahakamani kupaza sauti za juu na hali za kihisia kama vile hoja za waathiriwa mahakamani, ambapo waathiriwa wa ubakaji wanapokutana ana kwa ana na washambuliaji wao.
Hadi sasa Mbwa Lol amekuwa katika kesi 80 za uchunguzi wa uhalifu tofauti zilizowahusisha waathiriwa kuanzia miaka mitatu hadi wa miaka 90.
Post a Comment