CHANDE AWATAKA WACHIMBA DHAHABU KUTOTUMIA MAGOGO
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Hassan Chande amewataka wachimbaji wadogo wa dhahabu kutotumia magogo katika shughuli zao kwa kuwa ni chanzo cha ukataji wa miti.
Chande ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wachimbaji wa mgodi mdogo wa Sekenke One uliopo wilayani Iramba Mkoa wa Singida alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 katika shughuli za uchimbaji.
Alisema kuwa imebainika wachimbaji wengi hukata miti kwa ajili ya kujengea mashimo lakini alitahadharisha vitendo hivyo huchangia kwa kiwango kikubwa uharibifu wa mazingira.
Aliwashauri watumie njia mbalimbali zikiwemo kujengea kwa zege mashimo hayo kwa kuwa ni salama zaidi na pia huepusha vitendo vya ukataji miti na hivyo kuendelea kuhifadhi mazingira.
“Tumekuja hapa kutembelea mgodi wenu na tumeona harakati za uzalishaji wa madini ya dhahabu lakini nitoe wito kwa wamiliki wa migodi wenye leseni tuache kukata miti na kutumia katika mashimo tutumie zege na kwa kufanya hivyo tutapunguza ukataji miti,” alisema Naibu Waziri huyo.
Pamoja na kuendelea na shughuli hizo ambazo huwaingizia kipato alitoa wito kwa wachimbaji hao kushiriki katika uhifadhi wa mazingira ikiwemo zoezi la upandaji miti na kuitunza.
Pia, Naibu Waziri huyo alisema ni vyema wakawa wanafukia mashimo baada ya kumaliza uchimbaji kwani ni chanzo cha uharibifu wa mazingira na pia yanaweza kusababisha ajali lakini.
Kwa upande wake Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati, Dkt. Franklin Rwezumula alisema Serikali imekuja na mradi wa kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo.
Alisema mradi huo ambao umeanza kutekelezwa utaifikia migodi midogo mbalimbali nchini ukiwemo wa Sekenke One na utakuwa na manufaa makubwa kwani utawasaidia kujifunza namna ya kufanya shughuli zao pasipo kuharibu mazingira.
Dkt. Rwezumula alisema kupitia migodi ya mfano itakayojengwa katika baadhi ya maeneo nchini wachimbaji wadogo watajifunza mbinu bora za uchenjuji wa dhahabu bila kuathiri mazingira.
Aliwataka wenye kuendesha shughuli za migodi kusajili miradi yao katika Baraza hilo kwa mujibu wa utaratibu ili zitambuliwe na kusajiliwa.

Post a Comment