BALOZI BATILDA SALHA BURIANI AAPISHWA LEO IKULU MWAMWINO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 21 Juni, 2021 amemuapisha Balozi Batilda Salha Burian kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Aidha, Mhe. Rais Samia pia amemuapisha Zuwena Omary Jiri kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga. 

Akizungumza mara baada ya viongozi hao kuapishwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka viongozi hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Mhe. Majaliwa ametaka wasimamie huduma zinazotolewa na watumishi wao ili huduma hizo ziwe na ubora unaotegemewa na wananchi.

Ametaka kuhakikisha watendaji katika maeneo wanayokwenda kusimamia rasilimali fedha zinazokwenda katika mikoa yao ili zitumike kama zilivyokusudiwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Batilda Buriani kusimamia mapato katika Mkoa wake kwasababu kuna
baadhi ya wilaya katika mkoa huo hazifanyi vizuri katika ukusanyaji wa mapato.

Ametaka mbali na kusanya mapato hayo, wanatakiwa kuhakikisha fedha hizo zinatumika katika kuwahudumia wananchi katika huduma za jamii.

Aidha, kwa Mkoa wa Shinyanga amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo kusimamia vizuri matumizi ya fedha.

No comments