MAELEKEZO YA GERALD MWELI

Wakurugenzi wa Halmashauri zote Nchini kuhakikisha watumishi wote wenye Sifa za kupanda madaraja hususan walimu wawe wameingizwa kwenye mfumo ifikapo Juni 
12,2021.

Maafisa Elimu Wilaya 67 ambao Halmashauri zao hazijaanza kuingiza majina ya Walimu wanaotakiwa kupanda madaraja kwenye mfumo na wako kwenye mashindano ya Umisseta na Umitashumta warudi kwenye vituo vyao vya kazi na kufanya kazi hiyo kwa siku zilizobakia na mwisho ni Juni 12,2021.

Wakuu wa shule wawajengee uwezo wanafunzi wa kidato cha nne kujaza 'Selform' ili watoto waende kwenye tahasusi za ndoto zao.

Wakuu wa shule wawasisitize wazazi kuwa karibu na wanafunzi wakati wa kujaza Selform ili wakubaliane na watoto wao kuhusu machaguzi ya shule za kidato cha tano na vyuo.

Wakuu wa shule wajiandae kupokea wanafunzi wa kidato cha Tano Julai, 2021 na kwa zile Shule 42 zilizoongezwa mwaka huu wahakikishe zinakuwa na mazingira rafiki ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha Tano Mwezi Julai, 2021.

Wataalamu wa Elimu katika Halmashauri, Tume
ya Utumishi wa Walimu, Ukaguzi wa Elimu Kanda
wafanye kazi kama Timu na kutumia kwa pamoja
rasilimali zilizopo katika Halmashauri kama
Magari nk.

No comments