MENEJA MACHINJIO APEWA MIEZI MITATU
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ametoa miezi mitatu kwa Meneja wa Machinjio ya Dodoma, Victor Mwita kufanya maboresho ya miundombinu iliyopo katika machinjio hayo ili iweze kutoa huduma inayostahiki na kuchangia ipasavyo katika pato la taifa.
Ulega pia ametoa onyo kwa maafisa wa serikali ambapo hawatosimamia ukusanyaji wa mapato vizuri ambapo amesema afisa yeyote atakayeleta uzembe ataondolewa kazini mara moja.
“Natoa miezi mitatu (3) ya kuboresha miundombinu ya machinjio hii, na mimi nitakuwa nakuja hapa kila mwezi kuangalia ni maboresho gani mmeyafanya, madhumuni yetu machinjio hii iweze kutoa mchango unaohitajika kwa taifa.
Tuko imara sana katika ukusanyaji wa mapato, afisa yeyote asiyekusanya mapato ya serikali tutamtoa mara moja, tunataka tuhakikishe watu wanakusanya kwa haki na huduma inayotolewa pia itolewe kwa haki, hili jambo tunataka kulisimamia bila muhali,” Amesema Naibu Waziri Ulega.

Post a Comment