MAELEKEZO KWA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

Sekretarieti ya Mkoa ina wajibu wa kuzisimamia, kuzishauri na kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza na kutimiza majumumu yake
mkalisimamie hilo.

Tutaziimarisha Sekretarieti za Mikoa kwa kuhakikisha kuwa watumishi wa Ngazi hiyo wanauwezo mkubwa katika kushauri na kutoa mchango wa kuleta maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Tutatenga fedha kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ili Sekretarieti za Mkoa ziweze kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Ongezeni usimamizi na ufuatiliaji kwenye Miradi
inayotekelezwa kwa 'Force Account' ili kuhakikisha Miradi hiyo inajengwa kwenye ubora uliokusudiwa.

Kasimamieni ukusanyaji wa Mapato ya ndani
katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na kudhibiti
mianya ya upotevu wa mapato Wekeni Mkakati wa kuhakikisha tunafikia lengo ukusanyaji wa mapato tulilojipangia katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Simamieni Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha zinatenga fedha za mapato kwa
ajili ya kutekeleza miradi maendeleo inayotatua changamoto za wananchi ikiwemo elimu, afya na miundombinu ya barabara Simamieni Matumizi ya fedha za mapato ya ndani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hakikisheni matumizi sahihi ya fedha za Miradi ya Maendeleo zinazotoka Serikali Kuu. 
Mhe. Ummy Mwalimu(Mb)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI

No comments