KLABU YA SIMBA SC ILITUMA MWAKILISHI
Klabu ya Simba ilituma mwakilishi kwenye msiba wa mke wa mchezaji wetu Clatous Chama ambae ni Msaidizi wa Afisa Habari wa klabu, Ally Shatry. Msiba huo ulifanyika Kitwe nchini Zambia.
Pamoja na mambo mengine klabu ilipeleka rambirambi za awali kwa kiungo wetu huyo fundi.
Kwa upande wake Chama ameishukuru klabu, hususani Mtendaji Mkuu, menejimenti, bodi ya wakurugenzi, wanachama na washabiki wote wa Simba kwa salamu zao za pole na kuomba wazidi kumuombea yeye na familia yake ili wapate nguvu zaidi
(Via;@simbasc)
Post a Comment