JINSI YA KUPENDA
JINSIYAKUPENDA: Mtizamo wa Kibiblia.
Kama tukiacha vyazo vingine vyote , Biblia inasemaje kuhusu upendo¿
Nafikiri upendo ni neno linalozungumzwa Sana lakini ninmiongoni maneno yaliyoeleweka vibaya.Nafikiri hakuna kamusi inayomaliza( Exhaust) maana ya neno hili. Kitabu pekee kinachoelezea kikamilifu habari za upendo ni Biblia.[hasa.1Kor13:4-8: Huu wapaswa kuwa mzani kwa wote wanaopenda]. Katika lugha ya asili ya Kigiriki kilichotumika hapa, kanuni za upendo zinazotajwa hapa ziko katika ASILI YA KITENZI.Mungu alipotaka kuelezea upendo , alitumia kitenzi kwa sababu upendo ni kile unachofanya hasa zaidi ya vile unavyohisi. Utakumbuka tumekuwa tukijufunza upendo ni Nini&sio Nini. Lakini , _TUNAPENDAJE_ ¿
*Upendo ni Kutoa* : Kwa maana jinsi hi Mungu _aliupenda_ ulimwengu, hata *akamtoa* mwanawe pekee...Enyi waume , wapendeni wake zenu, kama Kristo _alivyolipenda_ Kanisa , *akajitoa* kwa ajili yake.[Yn3:16&Eph5:25]. Kristo anatuambia tuwapende adui zetu... Suleimani anatuambia jinsi ya kuwapenda anasema Adui yako akiwa na njaa , *mpe* chakula , Tena akiwa na kiu *mpe* maji ya kunywa.[Matt5:43-44&Mith25:21].
Nia Yako ni Muhimu Zaidi: Subiri kidogo⚠️Kama kupenda ni Kutoa, vipi kuhusu 1Cor 13:1-3?Aya hii inatukumbusha ukweli mchungu kwamba huduma, karama na kujikota koote katika ubora wake pasipo upendo ni bure.Kumbe unaweza Kutoa( yamkini hata maisha yako) pasipo kuwa na upendo.Ni kwa jinsi gani mtu ,aweza Kutoa mali zake zote kulisha maskini na akajitoa kufa kwa ajili ya wengine , halafu asiwe na upendo¿ Upendo sio Kutoa tu..ni kutoa kwa nia Safi.Kana utatoa kitu kw mategemeo ya kupata kitu , huo sio upendo kibiblia na unapoteza thawabu yako ya milele [ Mdo8:18-20;Matt6:2].Upendo wa kweli hutoa pasipo kutegemea chochote Kama malipo. Upendo halisi hauhitaji malipo ili uendelee kupenda.Okay! Upendo ni Kutoa pasipo kutegemea chochote in return.
*Unachotaka Vs Unachohitaji:* Je, umawahi kusikia kauli Kama hii? Kama unani🤍 inatakiwa kunipa *chochote ninachotaka*...Je, utampa chochote anachotaka?..Hapana , lazima ujifunze kutofautisha anachotaka (want) na anachohitaji(need). Katika utamaduni wa leo , mstari unaotenganisha Kati ya takwa na hitaji umeharibiwa Sana, hata ndani ya ukristo ambao wangepaswa kujua vema. Kama ukisoma kwa makini kisa Cha Yesu , Martha na Mariamu utagundua kuwa Martha alitaka dada yake amsaidie , lakini hitaji lake hasa likikuwa ni kukaa miguuni kwa Kristo na kusikia neno lake.[Luke10:38-42].Naamini hitaji kuu kabisa la mwanadamu ni [1] Kumpenda Mungu kwa moyo wake wote , akili zake zote ,nafsi yake yote na nguvu zake zote. Na [2]Kumpenda jirani yako kama nafsi yako mwenyewe [Matt22:36-40]. Mbali na hili mwanadamu ana mahitaji mengine ya msingi Kama vile mashauri ya Mungu kupitia neno, na chakula na maradhi ( cf.Mat4:4&1Tim6:8]
*Upendo katika muktadha wa ndoa ni kumpatia mwenzio kile Biblia inachosema anahitaji pasipo kuwa na kutegemea malipo yoyote. Ni vema kumpatia kile _anachotaka_ pia, endapo _kinapatana_ na maandiko matakatifu.*
*PCM 360°©2021™*
Post a Comment