BASATA YAMPONGEZA DIAMOND PLATNUMZ

Baraza la Sanaa Nchini Tanzania @basata.tanzania BASATA, imempongeza @diamondplatnumz, kuhusika katika kiny'ang'anyiro cha kuchukua tuzo ya BET.

#REPOST @basata.tanzania 

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linapenda kumpongeza Msanii Nasib Abdul (Diamond Platnumz) kwa kufanikiwa kutajwa kuwania tuzo za Black Entertainment television (BET) za mwaka 2021 katika kipengele cha Best International Act (Msanii aliyefanya vizuri kimataifa).

Haya ni mafanikio makubwa sana katika maendeleo ya Sanaa si kwa Diamond pekee bali kwa Tasnia nzima ya muziki wetu wa Tanzania. 

Hivyo Msanii akishinda tuzo hii Taifa zima linapata sifa; na hii ni njia moja wapo ya kuvutia uwekezaji kutoka ndani na nje ya Nchi na hatimae kukuza uchumi wetu.

Kwa nafasi hii; BASATA inatoa wito kwa wadau wa Sanaa na Wananchi wote kwa ujumla walio ndani na nje ya Nchi kumuunga mkono Msanii wetu ili afanikiwe kutwaa tuzo hii.

Washiriki wanaotajwa (Nominees) kuwania Tuzo hizi hupatikana kupitia "BET Voting Members" ambao ni jopo la watu waliopo kwenye Sekta ya Sanaa na Burudani na huangalia mambo yaliyofanywa katika Sanaa na Burudani) na Msanii husika ndani na nje ya Nchi.

Tuzo zinatarajiwa kutolewa tarehe 27 Juni 2021 huko Los Angeles Marekani.

No comments