IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Jana tarehe 31.5.2021 amefanya mabadiliko madogo kwa Makamanda wa Polisi ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, kumpandisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Camillius Wambura kuwa Kamishna wa Polisi na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)nna Kamishna Msaidizi wa Polisi Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi na kumteua kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Fedha na Logistiki.
1. Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Lucas Mkondya amehamishwa kutoka kuwa Kaimu Kamishna wa Fedha na Logistiki Makao Makuu ya Polisi Dodoma kuwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
2. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rufiji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga amchamishwa kwenda kuwa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto ambaye anastaafu.
3. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhan Ngh'anzi amehamishwa kutoka kuwa Boharia Mkuu kwenda kuwa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza.
4. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mwamini Rwantalenamehamishwa kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambako alikuwa
Mkuu wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Tazara.
5. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne Muliro amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuchukuwa nafasi iliyoachwa na Kamishna wa Polisi Camillius Wambura.
6. Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zuberi Chembera amehamishwa kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dodoma kwenda Makao Makuu ya
Polisi Zanzibar kuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai Zanzibar ambapo anachukuwa nafasi ya Kamishna wa Polisi Hamad Khamis Hamad
7. Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Stella Richard amehamishwa kutoka kuwa Kamanda wa kikosi cha Polisi Tazara kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.
Post a Comment