MALISA GJ ATAJA SABABU ZINAZOMKABIRI OLE SABAYA

Moja kati ya tuhuma zinazomkabili aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ni unyanyasaji wa kingono. Sabaya anadaiwa kulazimisha ngono wanawake mbalimbali, kuwachukua kwa nguvu anapokutana nao kwenye klabu za usiku, na kuwapeleka hotelini kufanya nao ngono kwa lazima. Jumla ya wanawake 40 wamejitokeza kutoa ushahidi TAKUKURU.

Kati ya wanawake hao wapo wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika mikoa ya Arusha na Kilimnjaro. Kati ya wanafunzi hao wawili wanadai kulawitiwa baada ya kutekwa na walinzi wa Sabaya walipokutana nae night club. Mmoja kati ya walinzi amekiri kuwapeleka wasichana hao kwa Sabaya lakini amekanusha tuhuma za ulawiti.

"Tuliagizwa kuwachukua lakini sikujua mahusiano yao na Mhe.Sabaya wala sikujua kama walikubaliana kukutana. Nakiri kuwapeleka kwake lakini kuhusu kulawiti siwezi kutoa ushahidi maana sikuwa naye ndani" mmoja wa walinzi wa Sabaya ameieleza timu maalumu (task force) inayochunguza suala hilo kwa kushirikiana na TAKUKURU.

Sabaya anadaiwa kufanya vitendo hivyo katika hoteli mbalimbali za kifahari jijini Arusha na amekuwa akiondoka bila kulipa. Baadhi ya hoteli zimekiri kumdai Sabaya baada ya kupata huduma mbalimbali ikiwemo malazi na chakula lakini amekua akindoka bila kulipa. CG Hotel wanamdai 8.7M, Grand Melia 14.8M, Melvis Hotel 3.4M, na Massai Land 9M.

Sabaya ambaye yupo mahabusu tangu May 25 mwaka huu, anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote ikiwa ataonekana ana kesi ya kujibu.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni jana alisema "Ni kweli tunamshikilia tangu jumanne ya wiki iliyopita kwa mahojiano ya tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka na rushwa. Akionekana ana kesi ya kujibu atafikishwa mahakamani"

No comments