TAARIFA KUTOKA YANGA SC

Uongozi wa klabu ya Yanga unawaarifu Viongozi wa Matawi na Wanachama wa Yanga kwa ujumla kwamba umeanza kupokea maoni juu ya Mfumo na Katiba pendekezwa kwa ajili ya Mabadiliko ya Uendeshaji wa klabu yetu.

Hivyo basi Wanachama wanatakiwa kujadili kupitia matawi yao na kisha kuwasilisha maoni na mapendekezo yao kwa Katibu Mkuu wa Yanga.

Mwisho wa kupokea maoni ni tarehe 20/06/2021 saa 11 jioni.

Uongozi wa Klabu unaendelea kusisitiza kwamba mapendekezo yaliyowasilishwa hayakuwa hitimisho hivyo ni vyema viongozi wa Matawi wakawashirikisha wanachama na wapenzi kadri
inavyowezekana ili kupata maoni mengi zaidi.

Maoni yanaweza kuwasilishwa moja kwa moja Ofisini Makao Makuu,Jangwani au kwa barua pepe info @yangasc.co.tz

No comments