HALMASHAURI KUTENGA MAENEO KWA AJILI YA VIWANDA VIDOGO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga maeneo maalum kwa ajili ya viwanda vidogo, wajasiliamli na shughuli nyingine za biashara ili kuwawezesha wananchi kujiari na kujiingizia kipato.
Akiongea na wafanyabishara wa eneo la Nzongomela katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda vidogo na wajasiriamali kunarahisisha kutambua wahitaji wa mikopo ya asilimia kumi inayotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kukopesha wajasiriamali wadogo.
Waziri Ummy anafafanua kuwa pamoja na kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda vidogo na wajasiriamali katika Halmashauri kutasaidia miji kupangika na kuweka mazingira ya miji kuwa masafi na kuvutia pia kuongeza mapato ya Halmashauri.
“Tunahitaji Miji yetu ipangike, tunahitaji miji yetu ivutie, tunahitaji miji yetu ipitike na kupendeza, hivyo ni vyema maeneo yakapangiliwa kwa umakini mkubwa kwa kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi” amesisitiza Waziri Ummy Mwalimu
Akizungumzia kuhusu eneo hilo Waziri Ummy ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa kutenga eneo lenye ukubwa wa ekari 200 kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na viwanda vidogo lililotengwa katika eneo la Nzongomela nje ya Manispaa ya Kahama.
Amezitaka Halmashauri kuweka utaribu wa kujifunza kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ni jinsi gani ilivyoweza kufanikisha kuwahamisha wajasiriamali na viwanda vidogo kutoka maeneo ya mjini na kuwapatia maeneo nje ya mji, lengo likiwa ni kuweka mpangilio bora wa miji
Aidha, eneo la Nzongomela lina wafanyabishara zaidi ya 1500 ambao waliamishwa kutoka maeneo ya Mjini ambapo wafanyabishara hao ni wauza mbao, mafundi milango, wapasua mbao, mafundi seremala, aluminium, Baba na mama lishe.

Post a Comment