FREDRICK MWAKALEBELA ASHINDA KESI
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela ameshinda kesi ya maombi ya marejeo mbele ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) dhidi ya hukumu ya kufungiwa miaka mitano kujishughulisha na mpira wa miguu ndani na nje ya Tanzania.
Kamati ya Maadili katika kikao chake cha Juni 23, 2021 ilisikiliza maombi hayo ya Mwakalebela na kukubaliana na sababu alizozitoa, hivyo kumuondolea adhabu ya kifungo cha miaka mitano pamoja na faini ya jumla ya sh milioni saba.
Mwakalebela katika maombi yake alisema anajutia kosa, hivyo anaomba aondolewe adhabu hiyo ambayo ameitii kwa kipindi chote.
Aliomba apewe fursa nyingine ya kuutumikia mpi
wa miguu kuahidi kuwa muadilifu kwa kufuata na kuheshimu sheria na kanuni zinazotawala mpira
wa miguu.
Vilevile Kamati ilikubaliana na maombi ya marejeo ya wanachama wawili wa Yanga; Bakili Makele na Boaz Ikupilika kufutiwa adhabu ya kufungiwa
miaka mitatu kila mmoja kwa kupinga kwa makusudi maelekezo ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ya namna ya kufanyika uchaguzi wa
klabu ya Yanga iliyotolewa na Kamati hiyo mwaka 2018.
Katika hatua nyingine, Kamati ya Maadili ya TFF imemfungia maisha Kocha Liston Katabazi kujihusisha na mpira wa miguu ndani na nje ya
Tanzania kwa kutoa shutuma za uongo dhidi ya TFF ambazo alishindwa kuzithibitisha.
Adhabu dhidi ya Katabazi imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 73(4) ya Kanuni za Maadili za TFF. Haki ya kukata rufaa kwa Kocha Katabazi iko wazi.
Post a Comment