MAKALA AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUVAA BARAKOA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amewataka Wakazi wa mkoa huo kuchukua tahadhari dhidi ya wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona, kwa kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka mara kwa mara.
 
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Makalla amewataka Wafanyakazi wa taasisi mbalimbali na watu wanaotumia usafiri vya umma kuepuka msongamano.
 
Amewataka wakazi hao wa mkoa wa Dar es salaam kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya endapo watahisi dalili za corona, na amesisitiza watu kufanya mazoezi na kula mlo kamili.
 
Makalla ameyataja makundi ya watu ambayo yapo hatarini kupata maambukizi ya corona kuwa ni wazee na watu wenye magonjwa sugu kama shinikizo la damu, kisukari, figo, kifua kikuu na magonjwa ya moyo.
 
Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es salaam amewaagiza wakuu wa wilaya zilizopo mkoani humo, Wakuu wa taasisi za Serikali na binafsi na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kusimamia maelekezo hayo.

No comments