AMKA NA BWANA LEO 22
KESHA LA ASUBUHI
Jumanne 22/06/2021
*KUPENDA NI KUTUMIKA*
*Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu; tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu.* *1 Petro 1: 3, 4*
*Dini ya Yesu Kristo ina maana zaidi ya kuzungumza. Haki ya Kristo inajumuisha matendo sahihi na matendo mema yanayofanywa kwa usafi bila ubinafsi*. Haki ya nje, wakati uzuri wa ndani unakosekana, haitafanikisha chochote. “Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake.
*Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.” (1 Yohana 1: 5—7)*. Kama hatuna nuru na upendo wa Mungu, sisi si watoto Wake. Kama hatukusanyi pamoja na Kristo basi tunatawanya. *Sisi sote tuna mvuto, na mvuto huo una athari kwa majaliwa ya watu wengine, kwa ajili ya mema yao ya sasa na ya wakati ujao, au kwa ajili ya kupotea milele.*
*Sote tuna masomo ya kujifunza katika shule ya Kristo*, ili kufanya tabia za Kikristo ziwe kamilifu nasi ni wamoja pamoja na Kristo. Yesu aliwaambia wanafunzi wake, *“Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 18:3). Aliwaelezea maana yake.Hakutaka wawe watoto katika ufahamu bali katika uovu. *Watoto wadogo hawaoneshi hisia za ukuu na utawala. Wako sahili na halisi katika mwonekano wao.*
*Kristo angependa wafuasi wake wakuze tabia zisizoathirika, ili mwonekano wao wote uwe wa upole na unaofanana na Kristo.* Amefanya uwe wajibu wetu ili tuishi kwa ajili ya mema ya watu wengine. *Alitoka katika makazi ya kifalme ya mbinguni kuja katika dunia hii, ili kuonesha jinsi alivyokuwa anampenda mwanadamu*, na gharama isiyo na kikomo aliyolipa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu huonesha kwamba mwanadamu ni wa thamani sana kiasi kwamba Kristo aliweza kuacha utajiri Wake na heshima katika kiti cha mfalme ili amtoe katika uharibifu wa dhambi.
*Ikiwa Mkuu wa mbinguni angeweza kufanya kitu kikubwa hivyo ili kudhihirisha upendo wake kwa mwanadamu, ni kitu gani ambacho mwanadamu hatakuwa tayari kukifanya kwa ajili ya mwanadamu mwenzake ili kusaidiana kutoka katika shimo la giza na mateso?*
*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*
Post a Comment