AMKA NA BWANA LEO 10

```KESHA LA ASUBUHI

ALHAMISI, JUNI, 10, 2021
SOMO: WAKATI WA MAVUNO 

Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. 

Warumi 13:11, 12. 

Tunaunda sehemu ya mfumo mkubwa wa jamii ya wanadamu, na ushawishi unatoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine, si tu kanisani bali pia katika familia ya mbinguni na familia ya duniani huchangamana, ili kwamba Kristo awe nguvu katika ulimwengu. Madini ya thamani ya ukweli uliotolewa kwa wazee na manabii, ambao umejikusanya kuanzia enzi na enzi, na kutoka kizazi hadi kizazi, unapaswa kukusanywa kama amana za urithi.

Ushawishi mtakatifu wa vizazi vya sasa na vilivyopita huunda wakala imara na wenye nguvu kwa ajili ya Mungu, unaoweza kusimama si dhidi ya damu na nyama, bali dhidi ya mamlaka na nguvu, na roho wa uovu katika sehemu za juu. Watu wa Mungu wa siku za leo wana upendeleo na fursa zote kuliko vizazi vilivyopita na nuru zaidi ili kuwafanya wawe na nguvu za ziada katika kazi ya Mungu kuliko ilivyokuwa kwa watu wa vizazi vilivyotangulia. Fursa hizi zinahitaji marejesho yake. Kwa upatanifu na hazina zetu za mbinguni tunaweza katika jitihada zetu kufungua njia mbele ya wengine. 

Bwana yu karibu. Viumbe wa mbinguni wakiunganika na ushawishi uliotakaswa wa duniani wanapaswa kutangaza ujumbe wa malaika wa tatu na kutangaza onyo. Mwisho wa mambo yote umekaribia. “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.” (Waebrania 10:37). Watu wanapaswa kujiandaa kusimama katika siku ya Bwana, na baada ya yote, watasimama. Wale ambao wanarundikana wanapuuzia kueneza ushawishi wao, kwa kuueneza mbali zaidi na zaidi, wakifika katika sehemu za mbali kabisa za ulimwengu wanapuuzia kusimama katika sehemu yao ya kazi.... 

Katika ombi Lake kwa wanafunzi wake muda mfupi kabla hajapaa, Kristo alisema, “Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.” (Yohana 17:20, 21). Hebu maneno haya mazuri yaandikwe kwa kidole cha Mungu kwenye kila moyo.

—Manuscript 7, Juni 10, 1891., “Huduma ya Kikristo katika Kanisa Hai.```

No comments