SHANGWE KATIKA NJIA YAKE SIKU YA 3

❣️ MASOMO YA MKUTANO MKUU KIZOTA DODOMA ❣️
"""
""""

❣️TRH. 09/06/2021.

❣️KAYA NA FAMILIA.

❣️SOMO: NJIA ZA KUTAFUTA MWENZI WA MAISHA.

Leo tunaendelea na masomo yetu kwa kuangalia njia za kutafuta mwenzi wa maisha. Ziko njia nyingi ambazo kila mtu anaweza kuwa nazo lakini leo ziko njia nne zilizotumiwa na Adamu za kupata mwenzi wa maisha.

Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. 
Mwanzo 2:18

Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake. 
Mwanzo 2:19

Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye. 
Mwanzo 2:20

Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, 
Mwanzo 2:21

na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. 
Mwanzo 2:22

Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. 
Mwanzo 2:23

Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. 
Mwanzo 2:24

Kazi ya kutafuta mwenzi ni ya Mungu. Tunatumia moyo kupenda na akili inatumika kuchagua mwenzi wa kuwa naye usitumie moyo kuchagua mwenzi.

Hakikisha unaziba mianya ya shangwe..

Mambo au njia za msingi za kuzingatia kwa mujibu wa Mwanzo 2:18-24.

1. Uhusiano (kufanana) mfano katika mambo gani? 

a)Umri ya umri ni muhimu. Lazima ujue mtu wa rika lako mzee usio binti, au binti kuolewa na mzee kuna vitu vitapungua katika maisha ya ndoa.

b) Daraja la kijamii. Tafuta wa daraja lako na siyo tofauti sana.

c) Elimu. Kadiri elimu inavyoongezeka ndivyo mtu hubadilika hivyo hakikisha mnaendana katika masuala ya elimu. Zingatia sana usipuuzie jambo hili.

d) Rangi na utaifa. Zingatia sana katika hili pia unapokuwa katika ndoa ya mataifa mawili pia uwe tayari kubebeana changamoto ndani yake.

e) Zingatia ufanano wa dini.
Mwanzo 2:18-20.

f) Zingatia tabia ya unayepanga kumwoa au kuolewa naye.

Usichukue yeyote tu hakikisha mnafanana wote katika mtazamo wa mambo ya kiroho, Kiakili.

2. Tumia kanuni ya mchujo. Yaani unaanza na kundi kubwa la watu hadi la chini unalolichagua. Kundi la kijamii. Hivyo ukishaona hivyo sasa unachuja kwa kuangalia mvuto wake ikiwa ukimwangalia utamwangalia tena. Lakini usivutiwe na vitu vya muda mfupi angalia vya kudumu katika maisha yenu yote. Baada ya hapo unaangalia utengamano wenu kama uko sawa.

Na hatua ya mwisho ni Fidia. Mfano ana udhaifu huu na mazuri haya ili yaweke uwiano sawa kati yenu. Hivyo nadharia hii ni njema.

3. Mvuto wa mwanzo.(First impression) usitumie mvuto wa mwanzo kufanya uamzi wa kudumu nenda hatua nyingine. Zingatia upendo wa mara ya kwanza, ndipo hatua ya maadili utafiti maadili yake yakoje? Hivyo  hatua ya kwanza huendeleza hatua zingine za utafiti. Uchambuzi wa mjukumu na mahali pa kuishi.

4. Kulala usingizi. Mwachie Mungu akuchagulie mwenzi wa maisha kwa maombi mengi nawe utafanikiwa.

🙏🙏🙏🙏

❣️NENO KUU.

❣️TRH. 09/06/2021.

❣️MCH. MARK WALWA MALEKANA.

❣️SOMO: KWANINI MAHANGAIKO MAKUBWA NAMNA HII?

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 
Mathayo 11:28

Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 
Mathayo 11:29

Mbona mahangaiko makubwa namna hii? Kila mahali ni vilio magonjwa vifo kwanini mahangaiko namna hii? Nani anasababisha mahangaiko namna hii? Si Mungu bali ni Shetani(jini, pepo, joka) geuza mtazamo huo Mungu hauwi watu wake. 

Shetani ni nini asili yake?

Tena neno la Bwana likanijia, kusema, 
Ezekieli 28:11

Mwanadamu, umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie, Bwana MUNGU asema hivi; Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri. 
Ezekieli 28:12

Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. 
Ezekieli 28:13

Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. 
Ezekieli 28:14

Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. 
Ezekieli 28:15

Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto. 
Ezekieli 28:16

Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama. 
Ezekieli 28:17

Hiyo ndiyo ilikuwa hadhi yake. Mungu aliumba mwanadamu mkamilifu, Mungu hakuumba shetani aliumba Malaika mzuri kabisa.

Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! 
Isaya 14:12

Sifa zake kabla ya kuasi: alikuwa Kerubi mwenye cheo cha juu akitoka Mungu yeye ndiye alifuata, alikuwa mzuri, mwaminifu, mwimbaji, akitembea katika mawe ya dhahabu, alikuwa mkamilifu alipoumbwa. Hivyo Mungu hakuumba maovu bali yalitokana na huyu Shetani.

Lusifa humaanisha mchukuaji wa mwangaza.

Je, nini kilitokea?

Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto. 
Ezekieli 28:16

Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama. 
Ezekieli 28:17

Kujiinua ndiko kulimwangusha shetani.

Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. 
Isaya 14:13

Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. 
Isaya 14:14

Kiburi, kujiona, ubinafsi, kujisifu ni mambo mabaya sana kwau mwanadamu maana ndiyo yalimwangusha Shetani toka mbinguni. Neno "MIMI" limewaangusha wengi leo katika maisha.

Matokeo yake yalikuwaje?

Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 
Ufunuo wa Yohana 12:7

nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 
Ufunuo wa Yohana 12:8

Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. 
Ufunuo wa Yohana 12:9

Shetani alitupwa chini.

Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo. 
Isaya 14:15

Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme; 
Isaya 14:16

Shetani alishushwa chini. Ezekieli 28:17-18.

Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
Ufunuo wa Yohana 12:12

Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. 
Luka 10:18

Ndipo akaja duniani.

Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? 
Mwanzo 3:1

Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; 
Mwanzo 3:2

lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. 
Mwanzo 3:3

Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 
Mwanzo 3:4

kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. 
Mwanzo 3:5

Tangu hapo ulimwengu ukaingia katika anguko la dhambi.

Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. 
1 Petro 5:8

Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; 
Warumi 5:12

maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; 
Warumi 5:13

walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. 
Warumi 5:14

Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo. 
Yohana 8:44

Matendo ya shetani anayopandikiza kwa watu ni haya:

Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 
Wagalatia 5:19

ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 
Wagalatia 5:20

husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. 
Wagalatia 5:21

Shetani ndiye chanzo cha maovu yote. Lakini tumaini liko wapi?

atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. 
1 Yohana 3:8

Waefeso 6:10-18.

Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. 
Yakobo 4:7

Shetani ataangamizwa milele zote.

Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. 
Ufunuo wa Yohana 20:9

Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. 
Ufunuo wa Yohana 20:10

Mateso hayatakuwepo tena.

Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili. 
Nahumu 1:9

Wito wa Mungu kwako na kwangu leo;

Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine. 
Isaya 45:22

❣️MUNGU ATUSAIDIE, PAMOJA NA MAHANGAIKO YOTE BADO NI SHANGWE KATIKA NJIA YAKE.

MUNGU ATUBARIKI SOTE.

No comments