VENANCE MABEYO ATEMBELEA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI
Jana Jumamosi tarehe 29 Mei, 2021. Mkuu wa Majeshi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, alitembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Jenerali Mabeyo yupo Nchini Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kumuaga Mkuu Majeshi wa Afrika Kusini Jenerali Solly Zacharia Shoke zilizofanyika kitaifa Jana Mjini Pretoria.
Kuhudhuria sherehe hizi, ni utaratibu uliowekwa na nchi wanachama wa Jumuiya za SADC ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika kuimarisha mashirikiano hususan katika Nyanja ya Diplomasia ya Ulinzi (Defence Diplomacy) na Amani katika eneo la nchi za SADC.
Jenerali Mabeyo, alikaribishwa Ubalozini na Mhe. Balozi Mej. Jen. Gaudence Salim Milanzi (Mst) na watumishi wa Ubalozi, Mhe. Balozi Milanzi alitoa taarifa fupi ya eneo la uwakilishi ya Afrika Kusini, Botswana na Falme ya Lesotho.
Katika taarifa hiyo, Mhe. Balozi alieeza kuwa hali ya uwakilishi inaridhisha kiulinzi na kiusalama, Ubalozi umeendelea kukuza mashirikiano na nchi za eneo la uwakilishi ikiwa ni pamoja na SADC. Kwa kufuata miongozo ya sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza kuendeleza Diplomasia ya kisiasa na kutekeleza Diplomasia ya uchumi.
Aidha, Mhe. Balozi alieleza kuwa hali ya UVIKO-19 iliathiri eneo la uwakilishi na athari kubwa imeonekana katika uchumi kama nchi nyingine duniani zilivyoathirika.
Mapema mwezi huu Afrika Kusini imeanza kuonyesha dalili za uchumi wake kutengamaa, kutokana na sarafu yake ya Rand kuimarika dhidi ya sarafu ya dola ya Marekani.
Post a Comment