DHAHABU ZAENDELEA KUSAFISHWA MWANZA
Imeelezwa kuwa tangu kuanzishwa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Mwanza, Precious Metals Refinery, jumla ya kilo 63.179 zimesafishwa kwa ubora wa asilimia 99.99.
Hayo yameelezwa leo na Mtaalam kutoka katika kiwanda hicho, Deusdedith Magala kwenye ziara ya Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula na Kamishna wa Tume ya Madini, Janeth Lekashingo waliyoifanya katika kiwanda hicho kilichopo Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.
Kiwanda hicho kinamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)na mwekezaji kutoka Dubai.
Mara baada ya kupata maelezo kutoka katika Kiwanda hicho, Profesa Kikula alipongeza utendaji wa kiwanda hicho na kuwataka watendaji wake kuendelea kuchapa kazi kwa bidii.
Katika hatua nyingine viongozi hao wa Tume wametembelea Ofisi ya Madini na soko la Madini Mwanza ambapo wametoa pongezi kwa watumishi wa Ofisi ya Madini Mwanza kwa kuvuka lengo la makusanyo ya maduhuli kwa asilimia152 katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Post a Comment