WATU 28 WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA WAYA WA UMEME KATIKA SOKO LA MATUNDA NCHINI DR CONGO

Takriban watu 28 wamefariki baada ya kupigwa shoti na umeme baada ya kukatika na kuanguka kwa waya wa umeme katika soko katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, polisi imesema.

Waya uliokuwa na kiwango cha juu cha umeme ulikatika ghafla na kuangukia ndani ya nyumba na watu waliokuwa wakinunua bidhaa (MATUNDA) Karibu na mji mkuu Kinshasa.

Picha ambazo hazijathibitishwa zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha hali baada ya tukio hilo, huku miili kadhaa ikionekana kwenye vidim bwi vya maji na haijawa wazi ni nini kilichosababisha kukatika kwa waya wa umeme.

"Tunaamini radi ilipiga sehemu ya waya huo, na kusababisha uanguke ardhini. Kampuni hiyo imetma salamu za rambirambi kwa familia za waathiriwa wa mkasa huo"-----> Kampuni Ya Taifa Ya Umeme Ya DRC 

"Kuanguka huko kwa waya kulitokea katika wilaya ya Matadi-Kibala iliyopo viungani mwa mji mkuu Kinshasa na kwamba watu kadhaa walifariki mara moja."-----> Jeshi La Polisi

No comments