USITUPE MTOTO

#UNAAMBIWA: Mchungaji Lee Jong-Rak kutoka Korea Kusini ametengeneza Kisanduku cha kuwekea Watoto ambacho kimeunganishwa na upande mwingine wa nyumba yake, lengo ni kwamba Watu wote ambao wanataka kutupa Watoto wao vichanga au Watoto wenye matatizo ya akili wawe hata kwa siri wanawaweka hapo badala ya kuwatupa Barabarani wakaishia kufariki Dunia.

Tangu mwaka 1998 Lee ameshawaleta Watoto wengi kuwaonesha upendo na kuwapeleka shule na anapambana na mambo yote ikiwemo kuwabadilisha diapers na kuwabmbeleza usiku wakilia akishirikiana na Mkewe na Wafanyakazi wachache, kwa saa anao Watoto zaidi ya 20 nyumbani kwake, mdogo kabisa ana miezi miwili na mkubwa miaka 18.

“Hauna haja ya kumtupa Mtoto asiye na hatia Kama umeshindwa kumlea mlete tutamtunza” ———Lee

No comments