RAIS SAMIA AKUTANA NA PROFESSOR SENAIT FISSELA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 31 Mei, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Miradi wa taasisi yabThe Susan Thompson Buffet Foundation Bi. Senait Fisseha ambayo inajihusisha na masuala ya afya ya wanawake.

Bi. Senat Fisseha amemueleza Mhe. Rais Samia kuwa taasisi hiyo ambayo imekuwepo hapa nchini kwa zaidi ya miaka 10 imetumia dola za Marekani takribani Milioni 90 (sma shilingi Bilioni 20 kufadhili miradi ya inayoshughulikia changamoto mbalimbali zinazohusiana na afya ya uzazi kwa wanawake na wasichana.

Amebainisha kuwa miradi hiyo imesaidia kukabiliana na vifo vinavyohusiana na ujauzito
kwa kuwawezesha wanawake kupanga wakati gani wa kupata ujauzito, wakati gani wa
kujifungua, kuepuka ujauzito katika umri mdogo na kujifungua salama.

Bi. Senait Fisseha ameshukuru kupata nafasi kuzungumza na Mhe. Rais Samia na amebainisha kuwa baada mazungumzo hayo taasisi hiyo ipo tayari kuendeleza miradinhiyo kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Kwa upande wake, Mhe. Rais Samia ameishukuru taasisi hiyo kwa mchango wake katika masuala ya afya ya wanawake hapa nchini na amemhakikishia kuwa Serikali ya Tanzania
ipo tayari kushirikiana nayo ili kukabiliana na changamoto zinawakabili wanawake na
wasichana katika masuala ya afya.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Doroty Gwajima na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale ambao baadaye wamefanya mazungumzo na Bi. Senait Fisseha kwa lengo la kujipanga namna taasisi hiyo itakavyofanya kazi na Serikali.

No comments