RAY C AMPA ZA USO DIAMOND PLATNUMZ
Kuanzia leo nimeokoka...Anyway kufupisha tu maneno...Tunachokizungumzia sasa ni uzalendo sio mtu binafsi!Na Uzalendo unaanza kwako mwenyewe !!!Ok kwa kifupi tu Lile cheko lako la Pepsizo la fiesta kwakweli lilinikera sana hasa ukizingatia show ilikuwa ya wasanii wenzio wa hapohapo Tanzania...(Ulikuwa sio uzalendo)
.Kuna kabati pale kwako limejaa matuzo makubwa makubwa.
Naamini Watanzania walichangia sana kujaza tuzo kwenye lile kabati kwa upendo na kujibana matumizi!wengine kujinyima hata chakula kuweka bando kuvote ututoe kimasomaso na kweli kwa upande wa kututoa kimasomaso muziki wetu kuheshimika barani Africa hilo umeliweza asilimia 150!!Yanayoendelea mitandaoni hasa twitter nadhani hata wewe huelewi mbona watu wameanza kuchange ghafla wakati miaka kama mitano nyuma watu tulikuwa hatuskii wala hatuambiwi kitu ni D D tu (mmoja wapo mimi)pitia posti za nyuma!!!!..nadhani hapo katikati ulikuwa unatuchamba sana !kama vile I got money more than you mazafantaz!(Sio Uzalendo)!!au zile interview za madongo kusanya wasanii wote Tanzania wafanye show na mimi nifanye show tuone nani atajaza.
(Sio Uzalendo) Kuna mda unakaa unajiuliza huyu dogo mbona hivi tena !Bora hata saivi unatupa break kidogo unawachamba Forbes (ingawa hata vile haipendezi kimataifa) Vichambo vyako vingi vimewagawanya mashabiki.Huo ni ukweli.PLS kuwa humble sasa..Na pia punguza machawa wa ajabu wanaropoka sana wanakera.Sema nini tunasonga mbele.Anza kufanya macolabo pia na wenzio hapo Bongo.(Na simaanishi wasanii wa WCB tu) Wengine ambao wanapambana na wanafanya vizuri kwenye Game!!!Washike mkono wenzio babaa utapata baraka zaid sababu Uzalendo uanzie kwako pia sio kwenye team yako tu .Au vipi babaa Nitaendelea kusapotii yeyote anaefanya poa na kwenye ukweli ntasema pia.Si ndio maana ya kuwa dada au.
Mpaka BUNGE limetushawishi kukusapoti na ni kweli tunakusapoti watanzania sasa basi tuendelee kubaki kwenye uzalendo huohuo kuwa na wewe pia wainue wasanii wenzio wengine kwa kushirikiana nao waonekane Africa ishangae na ione kuwa Tanzania kuna vipaji balaa! Anyway wabongo fanyeni kama mnajikuna mkavote tuchukue na hii tuzo.GO GET THEM GO Diamond Platnumz.
Post a Comment