AMKA NA BWANA LEO 1
KESHA LA ASUBUHI
JUMANNE, JUNI, 1, 2021
SOMO: MKRISTO WA KWELI
Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
Luka 4:10.
Mkristo wa kweli ni mtumishi wa Kristo. Kazi yake kwa ajili ya Kristo inapaswa kufanywa vizuri kwa ukamilifu. Hakuna kitu ambacho kitaiondoa akili yake kwenye kazi yake. Mambo mengine yanaweza kuangaliwa vizuri, lakini yakawa ni ya umuhimu mdogo, lakini huduma ya Kristo inahitaji mtu kamili, moyo, akili, roho, na nguvu. Hatakubali moyo uliogawanyika. Anatutarajia tufanye kadiri ya uwezo wetu. Na hakuna kinachofanywa kwa uaminifu kwa ajili yake ambacho hatakiona...
Kila mwanadamu anapaswa kufanya kazi aliyopewa na Mungu. Tunapaswa kuwa radhi kutoa huduma ndogo, tukifanya mambo ambayo yanapaswa kufanywa, ambayo mtu anapaswa kufanya, tukitumia vizuri fursa ndogo. Ikiwa hizi ndizo fursa pekee, tunapaswa kufanya kwa uaminifu. Mtu ambaye anapoteza saa, siku, na wiki, kwa sababu hayupo tayari kufanya kazi iliyopo mkononi mwake, ingawa ni duni kiasi gani, ataitwa kutoa hesabu kwa Mungu kwa ajili ya muda wake ambao wameutumia vibaya.
Ikiwa anahisi kwamba wanaweza kukaa bila kufanya kitu, kwa sababu hawezi kupata ujira anaoutamani, hebu aache na afikiri kwamba siku hiyo, siku moja hiyo, ni ya Bwana. Yeye ni mtumishi wa Bwana. Hapaswi kupoteza muda wake. Hebu afikiri, nitautumia muda huo katika kufanya kitu, na nitatoa chote nipatacho ili kueneza kazi ya Mungu. Sitahesabiwa kama mtu nisiyefanya kitu.
Mwanadamu anapompenda Mungu kwa kiwango cha juu, na jirani yake kama anavyojipenda, hataacha kuuliza ikiwa kila anachoweza kufanya kitamletea vingi au vichache. Ataifanya kazi, na kukubali ujira unaotolewa. Hataonesha mfano wa kukataa kazi kwa sababu hawezi kupata ujira mkubwa kama ambavyo alitarajia.
Bwana anaangalia tabia ya mtu kuhusu kile anachotenda katika kushughulika na wanadamu wenzake. Ikiwa katika shughuli za biashara za kawaida kanuni zake zina hitilafu, kanuni hizo hizo zitaletwa katika huduma yake ya kiroho kwa ajili ya Mungu. Nyuzi hizi zimesukwa katika maisha yake yote ya Kiroho. Ikiwa unadhani kuwa una hadhi kubwa sana kujifanyia kazi kwa ujira mdogo, basi mfanyie kazi Bwana, weka mapato yako kwenye hazina ya Bwana. Toa sadaka ya shukrani kwa Mungu kwa kuyalinda maisha yako. Lakini kwa namna yoyote usikae bila kazi.
—Manuscript 20, Juni 1, 1896,
Post a Comment