UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA SHINYANGA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu jana tarehe 28/05/2021 amefanya ziara katika Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuongea na Sekretarieti ya Mkoa na Kamati ya Fedha ya Mkoa na kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya Afya, Elimu na Miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Shinyanga

Akiongea na Sekretarieti ya Mkoa huo Waziri Ummy amesema kuwa Sekretarieti ya Mkoa ndio chombo cha kusimamia na kushauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutekeleza majukumu yao.

Waziri Ummy ameendelea kusema kuwa Sekretarieti za Mikoa zikitimiza wajibu wao zitazisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kutimiza majukumu yao ya kutoa huduma bora kwa wananchi

Amesema kuwa lengo la ziara yake ni kuwakumbusha wajibu wa Sekretarieti za Mikoa nchini kwa kuwa zikifanikiwa kutimiza majukumu yao kwa weledi itaisaidia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoa miongozo ya kisera na kutafuta fedha kwa ajili ya kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kutatua kero za wananchi.

No comments