WAZEE, WENYE ULEMAVU WATAKIWA KUPEWA KIPAUMBELE


Mkuu Ofisi anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt.Grace Maghembe amewataka watendaji wa vituo vya kutolea huduma kuangalia utaratibu bora wa kutambua watu wanaohitaji huduma za haraka  wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu pamoja na wajawazito kuanzia wanapoingia lango la Hospitali. Aliwataka pia kuweka utaratibu wa kuwalinda wazee.

Akizungunza wakati akikagua kituo cha Afya mbagala rangitatu tarehe 25.06.2021 amesema
Makundi hayo lazima yaoeee kipaumbele katika kupatiwa huduma bora za Afya

“Ukimuona mzee yupo katika foleni mpeleka sehemu husika ili apate huduma kwa utaratibu maalumu. Uzurio wa hapa kuna vijana waliovalia fulani ya’ niulize mimi ‘ambao wanatoa msaada mbalimbali.
 
Dkt. Maghembe amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa msongamano wa wananchi kukaa muda mrefu wa kusubiri matibabu kama alivyokutana nao wakati akikagua utoaji wa huduma katika hospitali hiyo.
 
Mmoja wa wagonjwa waliokuwa wakisubiri matibabu  Mwasiti Iddy, alimweleza Dk Magembe kuwa  changamoto kubwa katika hospitali ni watu kukaa muda mrefu licha ya kuwahi mapema kwa ajili ya kupata matibabu.
 
Akiwa katika eneo la Kimara Baruti kunakojengwa Hospitali ya wilaya ya Ubungo, Dk Maghembe alifurahishwa na namna ya ujenzi wa hospitali hiyo ya kisasa ulipofikia huku akiupongeza uongozi wa manispaa hiyo kwa kusimamia vyema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi ujao.
 
Pia aliwataka viongozi wa manispaa za Dar es Salaam, kuweka utaratibu bora kwa kukagua mchakato wa ununuzi wa vifaa tiba na vitendanishi  ili kujua mnyonyoro mzima wa hatua hiyo hadi kupatikana kwake. Amesemka hatua hiyo itasaidia kudhibiti udanganyifu huku akiwataka viongozi hao kushirikiana na waganga wakuu wa wilaya ambao wana utaalamu wa sekta hiyo.

No comments