SHERIA YA WAZEE KUTUNGWA NA KUFANYIWA KAZI

Rais Samia alisema anatambua wajibu alionao katika kuhakikisha sheria ya wazee inatungwa na kufanyiwa kazi jambo ambalo lipo katika mchakato kwa kuanza na maboresho ya sera.

Alisema sera za sheria hiyo zitakapokamilika hatasita kuharakisha mchako wa sheria yake kwakuwa anatambua umuhimu wa kulinda maslahi ya wazee nchini.

Pia alisema atazingatia maslahi ya kiuchumi, kwa kutoa fursa kwa wazee kuwezesha kupita miradi ya Mfuko wa Maendeleo wa TASAF.

" Katika TASAF sasa hatutakuwa na makundi wazee wote wenye sifa watanufaika,lakini kwakuwa miradi hii imefika mwisho upo mpango maalumu wa kuanzisha miradi mingine inayofanana na TASAF, "alisema.

Akizungumzia changamoto zinazowakabili wazee nchi Rais Samia alisema anatambua adha ya matibabu waliyonayo na amemuagiza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuchukua hatua za haraka.

Aidha kuhusu mgao wa pensheni kwa wazee wote, alisema kwa sasa nchi inapitia katika changamoto za kidunia kutokana na mtikisiko wa uchumi uliosababishwa na janga la Corona, hivyo wampe muda kwakuwa anatamani awe anatoa hata shi 30,000 kwa kila mzee kila mwezi.

Alisema, pamoja na nchi kufikia uchumi wa kati janga la Corona limesababisha uchumi kushuka kutoka asilimia 7 hasmdi

No comments