KUHUSU DSM, NIMEANZA KUCHUKUA HATUA

Akizungumzia sekta ya maji Rais Samia alisema katika Mkoa wa Dar es Salaam, ameanza kuchukua hatua ikiwemo kuongeza ufanisi wa miradi mikubwa miwili ya maji ili kumaliza adha iliyopo

Alisema lengo ni kuhakikisha Mkoa huo, unapata huduma ya maji kwa asilimia 100 na ameshasema na watendaji wake ikiwemo kuagiza kuchukuliwa hatua kwa mtendaji yeyote atakayehujumu miradi hiyo na kufanya ubadhilifu kwa kuongeza 'bill' kwa wateja.

"Nimesema na watendaji wa wizara, watu wasibambikiwe bill za maji atakayebambikiza ataondoka na bill zake lakini wananchi pia mkiletewa bill za halali lipeni,"alisema.

No comments