RAIS WA ZANZIBAR AFANYA TEUZI KWA WAKURUGENZI NA WENYEVITI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya Uteuzi wa Wakurugenzi na Wenyeviti katika Taasisi Mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma kama ifuatavyo:-

1) Ndugu Mshenga Mshenga Haidar ameteuliwa kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).

2) Ndugu Nassor Shaaban Ameir ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).

3) Ndugu Shariff Ali Shariff ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).

4) Dkt. Huda Ahmed Yussuf ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF).

5) Ndugu Suleiman Ame Khamis ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar.

6) Ndugu Hartha Mohammed Ali ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe.

7) Ndugu Abdulla Mzee Abdulla ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma.
Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 04 Mei, 2021.

No comments