RAIS SAMIA AMEPOKEA HATI ZA MABALOZI 5
Rais wa Jamhui ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 10 Mei, 2021 amepokea hati za utambulisho za Mabalozi 5 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi waliowasilisha hati zao ni Mhe. Lebbius Taneni Tobias Balozi wa Namibia Papa nchini, Mhe. Mary O'Nell (Balozi wa Ireland Japanchi, Mhe. Dkt. Mehmet Güllüoglu (Balozi wa Unmuki hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi (Balozi wa lowly hapur nchini na Mhe. Ricardo Ambrosia Sampio Mtumbuida (Balozi wa Msumbiji bajar
ncluind.
Mhe. Rais Samia amewakaribisha Mabalozi hao hapa nchini na kuwahakikishia kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana nao katika kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano na nchi hizo hususani katika masuala ya uchumi na ustawi wa jamii.
Ameongeza kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za uwekezaji katika sekta za kilimo, viwanda, utalii, ufugaji na uvuvi, hivyo amewaomba kuwaleta wawekezaji kutoka katika nchi zao kuja kushirikiana na Tanzania katika kuzitumia fursa hizo kwa manufaa ya pande mbili.
Aidha, Mhe. Rais Samia amewataka Mabalozi hao kufikisha salamu zake za shukrani kwa Marais wa nchi wanazowawakilisha na kuwahakikishia kuwa yupo tayari wakati wote kushirikiana nao.
Mabalozi hao wamemshukuru Mhe. Rais Samia
kwa kupokea hati zao za utambulisho na
kwa utayari wake wa kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano na Tanzania, na pia wamemuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha matarajio yake hasa katika uhusiano wa kiuchumi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mhe. Rais Samia kupokea hati za utambulisho za Mabalozi
tangu aingig madarakani tarehe 19 Machi, 2021.
Post a Comment