CHINA YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA ZANZIBAR

China yaahidi kushirikiana na Zanzibar katika ujenzi wa Uchumi wa Bluu kupitia uwekezaji wa Makampuni ya China katika uvuvi wa baharini na ujenzi wa viwanda vya kusindika bidhaa za baharini. Ahadi hiyo imetolewa leo katika Mkutano wa Ubalozi na Wizara ya Kilimo ya China.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa makubaliano baina ya Wizara ya Kilimo, Maliasili na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wizara ya Kilimo ya China yaliyosainiwa Mwezi Septemba 2018 wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

No comments