KAMPUNI YA LENOVO KUTOA FURSA KWA VIJANA WA TZ
Kampuni ya LENOVO Group ya China kutoa fursa kwa vijana wa Tanzania kupata mafunzo ya ufundi stadi kupitia programu yake ya Lenovo International Education Alliance (LIEA). Ahadi hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Idara ya Elimu wa Lenovo Bi.Jiang Yanan alipokutana na Balozi MBEL WAKAIRUKI.
Kupitia programu hiyo, vijana wa kitanzania watapatiwa mafunzo ya stadi za ufundi kwa kuzingatia mahitaji ya Makampuni yatakayokwenda kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali. Programu hiyo itafadhiliwa na Kampuni ya LENOVO na kuendeshwa na vyuo vya Ufundi vya China na TZ
Kampuni ya LENOVO ni miongoni mwa Makampuni Makubwa 500 duniani ikishikilia nafasi ya 224. Kampuni hiyo iliyojipatia umaarufu kwa utengenezaji wa bidhaa za elektroniki ina mauzo yaliyofikia Dola za Kimarekani Bilioni 50 kwa mwaka. Kampuni hiyo ina vituo 17 vya utafiti ulimwenguni

Post a Comment