PART 3 NA MWANZA NATURAL SKIN CARE
Mwaka 2006, tulihamia mtaa wa Shamaliwa katika kata hiyohiyo ya Igoma. Eneo hilo lilikuwa na ardhi ya kichanga na sehemu yake kubwa ilikuwa haijajengwa, wakazi walikuwa wachache. Japo eneo lilikuwa limepimwa lakini ofisi za jiji hazikuwa zimechonga barabara hivyo kila wakati mvua ziliponyesha maji yalisambaa na kusababisha mafuriko kwenye nyumba za watu. Siku moja, mama alikwenda ofisi za jiji na kuwasilisha kero yake hiyo kwenye ofisi ya maenginer ambao walimsikiliza bila kuchukua hatua yoyote ya utatuzi. Kero ile iliendelea kuwepo, mama hakukata tamaa, aliandika barua juu ya kero ya mafuriko na kuipeleka ofisi za jiji, lakini mara hii, kwenye ofisi ya Mkurugenzi. Baada ya kuipokea aliwaagiza maengineer ambao mwanzo hawakuchukua hatua kuwa walete mtaani kwetu greda na barabara na mitaro vichongwe mara moja. Siku walipoleta greda mtaani kwetu, badala ya kuanza kazi moja kwa moja, iliwabidi wapatafute nyumbani kwetu kwanza. Walimkuta mama na kuomba aonyeshe ramani ya barabara zote zilizotakiwa kuchongwa na hata walipomaliza kazi walimwuita tena mama ili akakague kazi yao. Kero ya mafuriko ilikwisha.
Wiki iliyopita watu wa jiji walifika nyumbani kwetu wakiandikisha nyumba zetu namba. Hii ni baada ya zoezi la kuzipa majina barabara ambalo linaelekea mwisho katika wilaya ya Nyamagana. Kupitia hili mama aligundua kuwa ofisi ya mtaa wetu haikufuata utaratibu, yaani haikuwashirikisha wananchi katika kuchagua majina ya barabara za mtaa wao. Majina yaliwekwa na watu wawili tu na majina hayo hayakuwa yakifaa kabisa. Mama aliamua kupiga simu kwa mtendaji wa kata na kuambiwa kuwa serikali ilikwishatoa agizo tangu mwaka jana kuwa wananchi wapewe nafasi ya kutoa majina lakini ofisi ya mtaa ilifanya uzembe hatimaye muda ukaisha. Baada ya kujua, mama alipeleka malalamiko yake ofisi ya mtaa mahali ambapo aliambiwa majina yalikwishapelekwa jiji na kwamba hakitabadilika kitu. Mama alianza kwenda nyumba hadi nyumba mtaani kwetu ili kuwaeleza watu kitu kilichotokea, aliwahamasisha watu kila kona kukataa majina yaliyotolewa bila ruhusa yao. Watu wengi walikubali lakini ikipofika asubuhi siku ya jumapili 2/5/2021, wengi hawakujitokeza.
Post a Comment