PART 2 NA MWANZA NATURAL SKIN CARE
Mama alifikiri "Je, mwalimu mkuu huwa anawaandikia hawa walimu ripoti gani ya kazi kila mwisho wa mwaka ikiwa katika maisha ya kawaida hawaelewani?" Mama alikuja na mpango madhubuti. "Chakula" chakula kingeweza kuleta amani. Mpaka muda huo walimu walikuwa wakishinda njaa shuleni au waliotaka kula ilibidi warudi majumbani mwao. Mama kwa pesa yake alinunua jiko la mafuta na vyombo pamoja na sukari na akaanza kupika chai kila siku kwa ajili ya walimu wenzake. Kila walipokutana kunywa chai mama alifanya usuluhishi kati yao, baada ya muda walimu walianza kutoa pesa zao kwa hiari ili chai iendelee kupikwa na mwisho wa mwaka huo walimu wote wa shule ya Itogwang'holo walishiriki sherehe ya pamoja ya kufunga mwaka.
Mwaka 2004 nilikuwa darasa la 2 katika shule ya msingi Montessori na wakati huo familia yetu ilikuwa imehamia Igoma (Mwanza). Kutoka mahali tulipokuwa tukiishi hadi kituo cha basi ilikuwa kama kilomita 2 na sehemu, umbali ambao ulituchosha sana mimi na wanafunzi wenzangu wa shule hiyo kwenda kusubiri school bus kila asubuhi na pia ilituchosha kwani tulikuwa tukiamka usiku sana. Mama yangu hakulipenda hili jambo na alipozungumza na wazazi wa wanafunzi wenzangu, walimueleza kuwa jambo hilo lisingeweza kubadilika kwani "Sister Dennis"(Mzungu, mkuu wa shule kipindi hicho) alikwisha kataa katakata kuruhusu basi la shule kuja karibu na maeneo ya nyumbani, alishaahidi kutobadilisha msimamo wake. Tuliendelea hivyo hadi mama alipoamua kwenda ofisini kwa mkuu huyo wa shule. Mazungumzo yalikuwa marefu mzungu yule akikataa kukubaliana na mapendekezo ya mama. Jibu lake lilikuwa "SIWEZI KUPELEKA GARI ZANGU PORINI." Jibu hili lilimuudhi mama na kwa hasira akamuuliza "IKIWA HUTAKI KULETA GARI KWANGU UNAKOSEMA NI PORINI, NI KWANINI BASI UNAPOKEA HELA NA WATOTO WETU WANAOTOKEA PORINI?" Mzungu yule alishtushwa na swali hilo na wafanyakazi waliokuwa pale kwa hofu walijaribu kumzuia mama wakimsihi asimjibu mkuu wao vile. Kulikaa kimya kwa muda kisha mzungu yule akaagiza mama aandike barua juu ya mapendekezo yake na akaagiza wasaidizi wake waifanyie kazi hiyo barua. Tangu siku ile gari ya shule ilikuja karibu kabisa na nyumbani.

Post a Comment