PART 1 NA MWANZA NATURAL SKIN CARE
KUHUSU MAMA:
Mama yangu (pichani) ambaye sitamtaja jina kwa sababu za kiusalama ni Mwanamke mwenye umri wa miaka 50 sasa.
KWANINI MAMA YANGU ANASTAHILI ZAWADI HII?
MAMA YANGU NI KIONGOZI WA HIARI.
Katika maisha yake yote, mama yangu hajawahi kuwa diwani wala hata mwenyekiti wa mtaa, lakini kwa miaka yote niliyomfahamu amekuwa kiongozi wa hiari. Kila mara amekuwa ngao, mtetezi na msimamiaji wa haki na usawa popote pale alipo. Ana kiu ya kuona maisha bora kwa kila mmoja. Mambo yale ambayo watu huyakimbia kwa kuyaona magumu kutatulika kwenye jamii, mama yangu husimama na kuonyesha njia hadi tatizo zikatatulika. Haya ni baadhi ya matukio ambayo mama yangu aliyavalia njuga na yakatatulika ingawa waliomtazama walimwambia kuwa hatoweza.
Mwaka 1996, mama alikuwa akifundisha katika shule ya msingi SUA. Katika shule hiyo kulikuwa na tatizo la walimu kuwalazimisha wanafunzi kusoma katika tuition zao kitu ambacho kiliwaumiza sana wanafunzi waliotokea familia maskini. Kulikuwa na mwalimu mmoja ambaye sitataja jina lake na kulikuwa na kijana Rajabu (Mwanafunzi mwenye akili sana darasani lakini maskini). Mwalimu huyo alimchukia sana Rajabu kwani japokuwa hakusoma tuition ya mwalimu huyo, bado alishika namba moja na kuwazidi wanafunzi waliosoma tuition yake. Siku moja, mama alimsikia mwalimu huyo akisema kuwa kwa mbinu yoyote angehakikisha kuwa Rajabu anafeli mtihani. Siku ya mtihani mwalimu huyo alichana karatasi ya Rajabu kwa makusudi akimsingizia kuwa alikuwa akiibia majibu. Rajabu alilia machozi huku akimuelea mama kitu kilichotokea. Mama aliamua kuyafikisha yote kwa mwalimu mkuu wa shule ambaye aliitisha kikao cha walimu wote haraka. Katika kikao hicho, Mwalimu huyo aliagizwa kutunga mtihani maalum kwa ajili ya Rajabu ili afanye upya. Katika mtihani huo Rajabu alipata asilimia mia moja ya maksi zote na akawa wa kwanza tena. Mbinu ovu ya yule mwalimu haikufanikiwa.

Mama alihamishiwa Kahama Shinyanga mwaka 1998 ili akafundishe katika shule ya msingi "Itogwang'holo". Alikutana na mgogoro mkubwa sana shuleni pale, walimu wakiwa na chuki na kutokuwa kabisa na maelewano na mwalimu mkuu wao.
Post a Comment