MAJALIWA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUWEKEZA KWA VIJANA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini katika mahubiri yao waweke msisitizo katika masuala ya kuwekeza kwa vijana ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo vyote hatarishi visivyozingatia maadili ya Mtanzania.
“Tusisahau pia kwamba ukimwi bado upo. Aidha, vijana wengi wapo katika hatari ya kupata maambukizi. Kwa Msingi huo, tumieni nafasi yenu katika jamii kutoa ushauri nasaha na hatimaye kupunguza kasi ya maambukizi kwa vijana”.
Ameyasema hayo Jana (Jumapili, Mei 9, 2021) katika ibada ya kusimikwa kwa Askofu Dkt. Msafiri Mbilu, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Lushoto. Waziri Mkuu ameshiriki ibada hiyo kwa niaba ya Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Amesema Serikali inatambua na kuthamini kazi na majukumu makubwa ya Viongozi wa Kanisa ambayo ni pamoja na kuwaongoza watu kiroho na kuwapa mafundisho, ushauri na kuwajenga kiimani.
Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi hao waendelee kutoa mafundisho yenye kuhimiza wananchi wadumishe amani na utulivu nchini kwa manufaa ya vizazi vya sasa na ya vizazi vijavyo.
Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali inatambua kwamba maendeleo ya nchi hayawezi kwenda bila ya ushirikiano na sekta binafsi na kwa kuzingatia hayo, imekuwa ikishirikiana na Sekta binafsi zikiwemo Taasisi za dini katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi na kuleta maendeleo ya Taifa.

Post a Comment