BYABATO AAGIZA KITUO CHA kV220/33 KUKAMILIKA HARAKA
Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato ameagiza kuwa, ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme cha kV 220/33 katika Kituo cha umeme cha Mtera ukamilike kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
Alitoa agizo hilo tarehe 9 Mei,2021 wakati alipofanya ziara katika kituo cha kufua cha umeme cha Mtera na kukagua sehemu ya Bwala la Maji la Mtera, kazi ya uzalishaji umeme na maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kipya cha kupoza umeme ambapo aliambatana na Watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na TANESCO.
“Tunapanua kituo cha kupoza umeme kilichopo hapa ili kukiongezea nguvu na hivyo kuweza kusambaza umeme katika Mkoa wa Iringa na Dodoma, kazi ilichelewa kidogo kutokana na masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa vifaa vya umeme kutoka nje ya nchi, hivyo nimetoa maelekezo kuwa Mkandarasi anatakiwa kufanya kazi usiku na mchana.”Alisema Wakili Byabato
Alieleza kuwa, tayari baadhi ya kazi zimeshafanyika katika kituo hicho kipya cha kupoza umeme ikiwemo ujenzi wa miundombinu na ufikishaji wa transfoma na vifaa vingine vya umeme vinavyohitajika.

Post a Comment