USHAURI KWA HARMONIZE

KUTOKA KWA BONGO TRENDING HABARI
Muziki ukiacha kuwa sanaa ni ajira, ukiacha kuwa Ajira ni sehemu ya Uwekezaji mkubwa, na kila mwekezaji huwa anawekeza ili mwishoni apate Faida. Nahisi pia lengo la Lebo ya Kondegang ni kuwekeza na sio tu kusaidia wengine, maana ingekuwa kituo cha misaada basi angesaidia wasanii wote Tanzania, ila kaweka Utaratibu wa Lebo kuna mikataba pale. Sasa niko ila naona hasara kubwa inaweza kutokea Kwa Kijana wetu na watu wanapaswa kujua hilo Ukiachana na ushabiki wa kinazi.

Msanii anapotoa wimbo hua analenga kuuza bidhaa yake kwa ukubwa, na sehemu za kuuzia huo muziki ndio hizi YouTube, BOOMPLAY, Spotify, AudioMack ITunes na sio Comment za mashabiki za kusifia au Kukandia. Sasa Narudi kwenye Mada Msanii kama Harmonize anatoa wimbo kwa Producer wa Audio kuna malipo, Anaenda Kushot Video analipa anapandisha YouTube miezi anapata Views Milioni 2.6 sawa na shilingi Milioni 2 na Laki 6 za Bongo, BOOMPLAY unapata Laki tano, AudioMack Laki Saba, Itune Alafu Hamsini ukijumlisha Kapata Milioni 5 huku Wimbo ukiwa na Gharama ya Milioni 10 hapo kuna hasara ya Milioni 5, ambazo anaweza kurudisha laki tano kwenye show, anabaki na hasara ya Milioni 4.5. 

Kumbuka msanii huyo ametoa Nyimbo zaidi ya 20 kwa hasara zinazofanana mwisho wa siku anaendelea kutoa zingine kwa hasara ile ile ndani Kijana anafilisika taratibu ila hawezi kukwambia kwamba jamani nafilisika. Ikumbukwe hapo wasanii wake pia wanazalisha hasara pia na show hawana. Unaamua kwenda Nigeria just Because Diamond kaenda South unapoteza Pesa huku Zuchu anashow DarLive, kijana wako upo nae Nigeria bila sababu za msingi.

Ikumbukwe Sarah anadai taraka na anasema anataka wagawane Mali na pesa walizochuma wakiwa pamoja hapo ndio tatizo kubwa lipo endapo atajiroga kutoa taraka.

Najaribu kusema haya Just Because nampenda sana Harmonize nafanya kumkumbusha aangalie watu wanaomzunguka kweli wanamtakia Mafanikio au wanachumia Tumbo?? Maana mtu anaetumia Tumbo hawezi kukwambia ukweli yeye mradi lake Liende. Samahani kwa Mashabiki wa Kondegang Fatilia mauzo ya Lebo mutoa ushauri. Mnaweza kuona Kijana leo anatrend kumbe.

Utaoji wa Nyimbo Kondegang uwe na utaratibu jamani.

No comments