KESI YA MORRISON, YANGA YATOA TAARIFA

KUTOKA YANGA SC;
Klabu ya Yanga inapenda kuwaarifu Wanachama, Wapenzi na Mashabiki juu Maendeleo ya kesi dhidi ya Bernard Morrison ambayo inaendelea kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

Kwa mujibu sheria na taratibu za uendeshaji wa mashauri katika Mahakama hiyo klabu hairuhusiwi kuelezea mwenendo wa kesi mpaka
kesi itakapotolewa maamuzi.

Hata hivyo Yanga inapenda kuwataarifu, Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wake kwamba kilichochelewesha kuanza kusikilizwa kesi hiyo ni pingamizi la awali (Preliminary Objection) la Mamlaka ya CAS kusikil rufaa hiyo lililowekwa na mjibu rufani (Bernard Morrison)
likitaka kesi hiyo irudishwe nchini.

Baada ya Mahakama hiyo kusikiliza hoja za pande zote mbili juu yanpingamizi hilo, CAS imelitupilia mbali pingamizi hilo la Morrison, hivyo
itaanza rasmi kusikiliza kesi ya msingi kuanzia tarehe 02 mwezi Juni 2021.

Klabu inapenda kuwatoa wasiwasi Wanachama, wapenzi na Mashabiki wake kwamba inaendelea kupambania haki zake mpaka haki itendeke,
na Klabu itawafahamisha Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wake maamuzi yatakayotolewa na Mahakama hiyo.

No comments