WAZAZI WAWILI KIZIMBANI

Wazazi wawili wamekamatwa na polisi katika kijiji cha Ilbisil kaunti ya Kajiado Nchini Kenya kwa madai ya kumtendea vibaya mtoto wao wa kambo wa miaka 3.

Mtoto wa miaka 3 ana majeraha mwili mzima, yaliyosababishwa wakati wa kupigwa.

Mbaya zaidi, mama wa kambo Faith Wanja anatuhumiwa kumlisha kijana huyo kinyesi.

Picha moja ilionesha mwili wa mvulana wa miaka 3 ikiwa inaumiza sana, majeraha ya mwili pamoja na sehemu zake za siri ikiwa ushahidi wa mateso ambayo mtoto amepitia.

“Yuko na alama za kuumizwa katika uso wake, Yuko na alama za kucha, mdomo nje na ndani…. mtoto hawezi fungua mdomo vizuri. ”alisema Dk Daniel Sankale.

Wakazi wanasema baba wa mvulana Michael Kamau na mama yake wa kambo Faith Wanja wamekuwa wakimtendea vibaya mtoto huyo kwa muda na kwamba maafisa wa Wizara ya Afya ambao walikuwa wakishughulikia chanjo za polio katika eneo hilo ndio walioripoti suala hilo.

"Huyo mama alichapa mtoto eti kwa sababu amejiharia, wakati naenda  kuchungulia namkuta anampatia mtoto mavi," alisema Elizabeth Simiyu, mmoja wa majirani.

Kamanda wa Polisi kaunti ya Kajiado Daudi Loronyokwe alithibitisha kisa hicho na kuongeza kuwa wazazi hao wawili watafikishwa mahakamani

No comments