PROFESSOR JAY; TUMSAPOTI DIAMOND PLATNUMZ
Mwaka 2008 nilichaguliwa kuwania TUZO za MTV BASE ambazo zilifanyika katika jiji la ABUJA - NIGERIA, Nilikuwa nimechaguliwa kugombea Category Ngumu sana ya BEST HIP HOP ARTIST ambapo nilikuwa nagombea na The GAME, LIL WAYNE na msanii wa NIGERIA anaitwa 9ICE, Nilikuwa Msanii pekee kutoka TANZANIA na nilikuwa nimeambatana na Joseph Kusaga, Kelvin Twissa kutokana na Nafasinzao kwenye MUZIKI wa AFRIKA.
Kwa MFANO huu wa NIGERIA Nitumie nafasi hii ya muhimu kuwaomba WATANZANIA wote kwa umoja wetu tusimame pamoja na tumsapoti Kijana wetu Diamond Platnumz ambae ni msanii pekee wa TANZANIA na anasimama kidete kuiwakilisha TANZANIA kwenye TUZO kubwa za BET aweze kushinda AWARD hii kwa manufaa ya TAIFA letu, mlango wa DIAMOND ukifunguka, Mlango wa wasanii wa TANZANIA umefunguka.
Kwa kweli nilijua kabisa kuwa SITASHINDA kwenye nafasi hiyo kutokana na ubora wa wale watu nguli niliokuwa nashindana nao ila niliona hiyo ni nafasi yangu kubwa na ya kipekee ya kuitangaza nchi yangu na utamaduni wetu na nilivaa vazi ililowavutia wengi VAZI la KIMASAI na nilipewa Heshima kubwa ya kukabidhi TUZO kwa mmoja wa washindi. Kilichotushangaza sisi tuliotoka TANZANIA ni CAMPAIGN ya nchi nzima ya WANAIJERIA ya kuhakikisha msanii wao 9ICE anashinda TUZO hiyo na sio TUZO hiyo pekee bali TUZO zote ambazo Wanaijeria wanagombea, Ilikuwa ni KAMPENI kubwa ya nchi nzima.
KAMPENI hiyo iliongozwa na WAZIRI wao wa SANAA na UTAMADUNI sambamba na WAZIRI wao wa UTALII, Nia yao ilikuwa kuwauza wasanii wao wa nchi yao kwa TAIFA lao.
Mwisho kwenye Category yetu msanii 9ice alishinda mbele ya JAYZ, LILI WAYNE na Mimi, Binafsi sikuwahi kumsikia kabisa mpaka leo ni miaka 15 imepita sijui hata alishawahi kuimba kitu gani, Kwa mwaka huo zaidi ya asilimia 90 za AWARDS zilibakia Kwa WANAIJERIA.
Hii ina ni funzo kubwa sana kwetu Watanzania kuwa anaposimama MTANZANIA yeyote kugombea TUZO yeyote au jambo lolote Duniani ni lazima tusimame nae pamoja bila kujali Makundi yetu , Itikadi zetu, dini zetu wala makabila yetu maana hapo Inasimama TANZANIA na sio mtu mmoja mmoja.
Kwa MFANO huu wa NIGERIA Nitumie nafasi hii ya muhimu kuwaomba WATANZANIA wote kwa umoja wetu tusimame pamoja na tumsapoti Kijana wetu Diamond Platnumz ambae ni msanii pekee wa TANZANIA na anasimama kidete kuiwakilisha TANZANIA kwenye TUZO kubwa za BET aweze kushinda AWARD hii kwa manufaa ya TAIFA letu, mlango wa DIAMOND ukifunguka, Mlango wa wasanii wa TANZANIA umefunguka.
Mungu ibariki TANZANIA, Mungu mbariki Diamond Platnumz.
Post a Comment